Mahakama ya Tanzania inatekeleza miradi mbalimbali ya ukarabati na ujenzi wa Mahakama nchini kwa lengo la kuboresha miundombinu yake ili kuwa na mazingira wezeshi ya utaoji wa huduma ya utoaji haki kwa ujumla.
Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa Mikoa kadhaa nchini ambapo miradi mikubwa ya ujenzi wa Mahakama inaendelea. Kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Mahakama ya Tanzania inatekeleza jumla ya miradi mitano ya ujenzi wa Mahakama katika Mkoa huo; ikiwemo ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama, Kituo Jumuishi ya Utoaji Haki - Intergrated Justice Centre (pichani juu), Mahakama za Wilaya Chemba na Bahi na Mahakama ya Mwanzo Kibaigwa.
Aidha, hatua ya maboresho ya miundombinu ya majengo ya Mahakama nchini inalenga pia kusogeza huduma za haki karibu zaidi na wananchi ili kumuwezesha mwananchi kupata huduma kwa haraka kwa kupunguza umbali na gharama katika kutafuta huduma ya haki.
Ujenzi wa jengo la Mahakama ya mwanzo Kibaigwa ukiendelea.
Ujenzi wa Mahakama ya Wilaya ya Bahi ukiwa katika hutua za mwisho
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.