Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MWENGE wa Uhuru mwaka 2023 ulitembelea, kuzindua na kuweka jiwe la msingi miradi sita yenye gharama ya shilingi 11,395,727,405.77 wilayani Dodoma.
Taarifa hiyo ilitolewa na Katibu Tawala Wilaya ya Dodoma, Sakina Mbugi alipokuwa akisoma risala ya utii kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa mbio za Mwenge wa Uhuru Wilaya ya Dodoma katika uwanja wa Shule ya Msingi Chamwino jijini hapa.
“Mheshimiwa Rais; miradi iliyopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2023 ni sita. Miradi iliyowekewa jiwe la msingi ni mitatu, ujenzi wa shule mpya ya Awali na Msingi ya mchepuo wa kiingereza Dodoma, mradi wa Maji safi Nzuguni na ujenzi wa Barabara ya Nzuguni – Mahomanyika (KM 5). Mradi mmoja umezinduliwa wa ujenzi wa Kituo cha Afya Nkuhungu, mradi mmoja Kikundi cha Vijana Faru Leather Products umetembelewa na mradi mmoja wa upandaji Miti Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini. Gharama za miradi yote sita ni shilingi 11,395,727,405.77, shilingi 494,077,045.00 ni mapato ya ndani na shilingi 10,901,650,360.77 kutoka Serikali Kuu. Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa Kilometa 71.9” alisema Mbugi.
Kuhusu michango ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2023, alisema “Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ulichangiwa shilingi 73,351,600. Wananchi pamoja na watumishi shilingi 27,051,600.00, wilaya shilingi 40,000,000 na Taasisi na makampuni ya Umma shilingi 6,300,000” alisema Mbugi.
Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 unaongozwa na kaulimbiu isemayo “Tunza Mazingira, Okoa vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.