KATIKA harakati za kuunga mkono jitihada za Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye matumizi ya nishati safi ya kupikia, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule amegawa mitungi 1000 ya gesi ya kupikia kwa makundi mbalimbali ya jijini humo.
Hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo imefanyika leo Septemba 20, 2024 kwenye viwanja vya Nyerere Square Jijini Dodoma kwa lengo la kuhimiza utunzaji wa mazingira sanjari na kuboresha afya husuani za kina mama wanaotumia nishati hiyo kupikia.
“Mkakati umetengenezwa Katika kipindi cha miaka kumi kuanzia 2024 hadi 2034 ambao utatuongoza watanzania namna ambavyo 80% ya watanzania kufikia 2034 wawe tayari wanatumia nishati safi, kwa kuanza na makundi yenye watu wengi, taasisi zenye mikusanyiko mikubwa na zinazotumia nishati chafu kwa wingi” Amesema Mhe. Senyamule
Hata hivyo, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mh. Jabir Shekimweri, ametoa tathmini ya athari ya matumizi ya nishati chafu kwa afya.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.