SHULE ya sekondari Miyuji inatekeleza mradi wa ujenzi wa madarasa mawili, ofisi moja ya walimu pamoja na kununua samani mradi ambao utasaidia kuongeza miundombinu ya kufundishia, kuondoa adha ya viti na meza, kuongeza idadi ya wanafunzi wapya pamoja na ufaulu kwasababu wanafunzi watakuwa wakisoma na kukaa kwa nafasi.
Hayo yalisemwa na Katibu wa kamati ya usimamizi na utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa madarasa mawili, ofisi moja ya walimu na ununuzi wa samani Mwalimu Rashid Abdallah alipokuwa akikagua maendeleo ya mradi huo unaotekelezwa katika shule ya sekondari Miyuji iliyopo kata ya Mnadani, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Rashid alisema kuwa shule yake ilipokea shilingi 40,000,000/= kutoka serikali kuu tarehe 2/10/2022 kwa lengo la ujenzi wa madarasa mawili, ofisi moja ya walimu pamoja na ununuzi wa viti na meza kwaaajili ya wanafunzi. “Baada ya kupokea fedha hizi tulifanya mchakato wa kumpata fundi ambapo tulitoa tangazo kwaajili ya kuwapata wazabuni na walijitokeza watatu ambao ni Jabir Athuman, Mark Victor pamoja na Mhidin Isack lakini kulingana na vigezo na masharti tuliyoweka kama kamati kwaajili ya kumpata fundi basi alipitishwa mtu mmoja ambaye ni Mhidin Isack. ikiwa ujenzi huo ulianza mnamo tarehe 13/10/2022 baada ya iliundwa kamati ya watu 15 na iligawanyika sehemu tatu ikiwa ni kamati ya mapokezi, manunuzi pamoja na usimamizi na utekelezaji kwa lengo lengo la kurahisisha majukumu.
“Kwa sasa ujenzi unaendelea na kuta zishapandishwa na leo tunatarajia kuingia katika hatua ya kuweka lenta (bimu), na mradi wetu umefikia asilimia 60% ya utekelezaji wake na mradi huu unatarajia kukamilika ifikapo tarehe 15/11/2022 ndipo utakapokabidhiwa,” alisema Abdalllah.
Ikumbukwe kuwa shule ya sekondari Miyuji ilianza tarehe 2/5/2006 ikiwa na wanafunzi 80, walimu wawili na vyumba vitatu vya madarasa, kwa sasa shule ina jumla ya vyumba 33 vya madarasa kati ya hivyo vinne vinatumika kama ofisi za walimu na maabara, wanafunzi wapo 1295 ikiwa wasichana 724 na wavulana 571 na jumla ya walimu 62, walimu wa sayansi na hisabati 12, sanaa 39 na biashara 04 na fundi sanifu wa maabala 01.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.