SERIKALI ya Tanzania imeingia makubaliano ya awali na kampuni kubwa za uchimbaji mafutaduniani zikiwemo Equinor na Shell kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa mradiwa uchakataji na usimikaji gesi asilia wenye thamani ya Dola za MarekaniBilioni 30 sawa na Shilingi Trilioni 70.
Makubaliano hayo ya awaliya mkataba wa nchi hodhi (HGA) yamefikiwa ikiwa ni zaidi ya miezi sita tanguSerikali irejee tena majadiliano na wawekezaji hao Novemba mwaka jana baada yaRais Samia Suluhu Hassan kueleza kuwa anataka kuona mradi huo ukiendelea kwamanufaa ya Watanzania na wawekezaji.
Katika hafla iliyofanyikaIkulu jijini Dodoma Juni 11, 2022, kampuni hizo mbili zimeingia makubalianohayo na Serikali kwa niaba ya wawekezaji wengine katika mradi huo ambao niOphir Energy, Exxon Mobil na Pavilion Energy.
Waziri wa Nishati JanuaryMakamba amesema hatua iliyofikiwa ni muhimu katika utekelezaji wa mradi huo wakuchakata na kusindika gesi asilia utakaojengwa mkoani Lindi ikiwemo hatua yauamuzi wa mwisho wa kiuwekezaji (FID) mwaka 2025.
“Mazungumzo hayakuwamapesi sana...kuna nyakati mambo yalitaka kuvunjika lakini ndiyo katikakuelekea kujenga...baadhi ya mambo yanayotakiwa yafanywe mbele yapo kwenye HGAhii,” amesema Makamba aliyeanza kuingoza wizara hiyo Septemba 2022.
Hatua ya kusaini mkatabahuo uliosainiwa na Wizara ya Nishati pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli(TPDC) pamoja na wawekezaji hao inatoa mwelekeo wa kutekeleza mradi huo ambaomazungumzo yake yalikuwa yamekwama kwa muda mrefu sasa.
RaisSamia amesema pamoja na kusaini mkataba huo wa makubaliano ya awali bado kunasafari ndefu kufikia uamuzi wa mwisho wa kiuwekezaji (FID) mwaka 2025 hivyowote wanaohusika katika jambo hilo waongeze kasi ya majadiliano.
Rais Samia amesema nchizote zenye rasilimali za gesi zimepata mafanikio ya kiuchumi na ni mategemeoyake kuwa Tanzania nayo itapata maendeleo na ustawi wa watu wake kupitiarasilimali zake.
“Natumaini kuwa kanuni zakimataifa zitazingatia masuala haya katika majadiliano yanayoendelea ilikuhakikisha Tanzania inaingia vyema kwenye ramani ya dunia ya wazalishaji gesina mazao ya gesi,” amesema Rais Samia.
Mradi huo unatarajia kutoaajira 10,000 wakati wa ujenzi wake ambapo zitapungua hadi 500 utakapoanzakufanya kazi huku ukitajwa kuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa sababuutaongeza uhakika wa nishati na kuipatia nchi fedha za kigeni.
Wawekezaji hao wamesemawanaamini kuwa mradi huo utatekelezwa kutokana na hatua iliyopigwa hadi kufikiakusaini makubaliano ya awali hasa kipindi hiki ambacho mahitaji ya gesi asiliayamezidi kuongezeka duniani kutokana na ongezeko la watu na mahitaji ya nishatisafi.
Makamu wa Rais wa kampuniya Shell Tanzania, Jared Kuehl amesema gesi ya Tanzania itaweza kupata soko kwasababu ina hewa ukaa kidogo na ipo karibu na soko kubwa la gesi la Asia.
“Gesi asilia kutokaTanzania itaweza kufanikisha upatikanaji wa nishati safi isiyo na hewa ukaanyingi...huu ni wakati muafaka kutekeleza mradi huu na kuhakikisha kuwaunafanikiwa kulifikia soko kutimiza mahitaji ya sasa ya gesi,” amesema Kuehlambaye pia ni Mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.