Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MKOA wa Dodoma umempongeza na kumtakia heri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa siku yake ya kuzaliwa na kumtakia maisha marefu ili aendelee kuwaongoza watanzania.
Pongezi hizo zilitolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule katika halfa ya kumbukizi ya kuzaliwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyofanyika katika makao ya taifa ya kulelea watoto- Kikombo, Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Senyamule alisema “sisi Mkoa wa Dodoma tunatoa pongeza kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza umri akiwa na nguvu na afya njema na maono ya kuliongoza taifa. Chini ya uongozi wake tunafuraha na amani”.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma alimtaja Rais kuwa ni mtu mwenye hekima sana na mchapa kazi. “Mheshimiwa Rais ametujengea uhusiano mzuri ndani na nje ya nchi. Hakika uongozi wake umeifanya Tanzania kuwa nchi pendwa duniani. Ameonesha kuwa anapenda haki na amefanya kila mtanzania aone furaha ya kuwa Mtazania, amekuwa mpatanishi wa umoja wa kitaifa. Kazi kubwa anayoendelea kuifanya ni kulinda rasilimali za watanzania” alisema Senyamule.
Katika salamu za Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alisema kuwa Jiji la Dodoma linajivunia kazi kubwa inayofanywa na Rais ya uwekezaji akisema kwa Dodoma ipo katika moyo wa Rais.
Nae Mkuu wa Wilaya ya Chemba, Gerald Mongella alisema kuwa watanzania wanajukumu kubwa la kumuombea Rais awe na afya na maisha marefu ili aweze kutekeleza maono yake kwa watanzania.
Hafla ya kumbukizi ya siku ya kuzaliwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ilihudhuriwa na viongozi kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa mamlaka za serikali za mitaa, viongozi wa dini, vyama vya siasa na mwakilishi wa mfuko wa Abbot Tanzania.
MWISHO
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.