Na Hellen M. Majid,
Habari – DODOMA RS
MKOA wa Dodoma umeshika nafasi ya nne (4) kati ya Mikoa 26 katika uandikishaji orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024 ambapo ni miongoni mwa mikoa iliyovuka malengo hadi kufikia Oktoba 20, 2024.
Mkoa huu umefanya uandikishaji kwa asilimia 104 ambapo makadirio ya wapiga kura kwa mujibu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) 2024 ni 1,712,472 ambapo wanaume ni 822,972 na Wanawake ni 889,500 lakini mpaka kufikia tarehe 20, waliojiandikisha walikua 1,784,260 kwa wanaume 875,640 na wanawake 908,620.
Kwa upande wa Halmashauri, Dodoma Jiji imeongoza kwa uandikishaji na kuvuka malengo kwa kufikisha asilimia 128.79 kati ya Halmashauri zote 184 za Tanzania ambapo iliandikisha jumla ya wapiga kura 628,715 ikiwemo wanaume 312,850 na wanawake 315,865.
Hata hivyo, wito umetolewa na Mamlaka husika yaani Ofisi ya Rais TAMISEMI kuwa ni muhimu pia nguvu na mikakati iliyotumika katika uandikishaji ikatumika kuelekea zoezi la kupiga kura ili wananchi wote waliojiandikisha wajitokeze kupiga kura.
“Serikali za Mitaa, Sauti ya Wananchi, Jitokeze Kushiriki Uchaguzi”
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.