UONGOZI wa Kata ya Mkonze katika Halmshauri ya Jiji la Dodoma umetakiwa kuhamasisha wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) iliyoboreshwa ili waweze kupata matibabu bure mwaka mzima.
Kauli hiyo ilitolewa na mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dkt. Joseph Mdachi alipokuwa akiongea na timu ya wataalam wa Kituo cha Afya Mkonze na viongozi wa Kata ya Mkonze kikao kilifanyika katika kituo hicho.
Dkt. Mdachi alisema kuwa hali ya mapato ya Kituo cha Afya Mkonze inadorora kwenye CHF iliyoboreshwa na bima ya kawaida. “Diwani na maafisa watendaji wana wajibu wa kuwahamasisha wananchi ili wajiunge na CHF iliyoboreshwa kwa wingi. Tunatakiwa kumuhamasisha mtu akiwa mzima hajaugua. Uhamasishaji huo ufanyike kupitia mikutano ya mitaa na kata. Tunaongelea CHF iliyoboreshwa kwa sababu ina mlinda mwananchi akiwa mzima” alisema Dkt. Mdachi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.