MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amewataka wafanyabiashara kuwa waaminifu kulipa kodi mbalimbali za serikali ili zisaidie kujenga miundombinu mbalimbali ndani ya jiji hilo ikiwa ni pamoja na maboresho ya masoko likiwemo la Sabasaba ili liendane na hadhi ya Jiji.
"Hakikisha kwenye biashara yako umelipa kodi zote halali za serikali ambazo zipo kwa mujibu wa sheria lakini pia matumizi ya mashine za EFD kwani hili ni agizo la serikali kuwa kila mfanyabiashara atoe stakabadhi za mashine...tujitahidi kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika biashara zetu" alisema Kunambi.
Alisema Jiji la Dodoma linafanya ukarabati wa miundombinu ya barabara katika mitaa ya Jiji hilo, ambapo aliwakumbusha wafanyabiashara kutopanga bidhaa zao katika maeneo yasiyoruhusiwa ikiwa ni pamoja na kwenye barabara za watembea kwa miguu.
Tufuatilie pia kwenye kurasa zetu za mitandao ya kijamii: (Facebook: Dodoma Jiji, Twitter: @DodomaJiji, Youtube channel: Dodoma City TV)
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.