• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkurugenzi asitoke kwenye kituo chake cha kazi wakati vikao muhimu vinaendelea- Mhe. Mchengerwa

Imewekwa tarehe: July 29th, 2024

Na. James Mwanamyoto OR-TAMISEMI

WAZIRI  wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa ameelekeza Wakurugenzi wa Halmashauri wasitoke katika vituo vyao vya kazi wakati wa vikao vya Kamati ya Fedha, Bajeti pamoja na vile vya Usalama ili kusimamia kikamilifu masuala muhimu ya maamuzi na kudhibiti upatikanaji wa hati chafu katika Halmashauri.

Mhe. Mchengerwa ametoa maelekezo hayo wakati wa kikao kazi chake na wakuu wa wilaya wote nchini kilichofanyika katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani.

“Inaonekana sababu kubwa ya halmashauri nyingi kupata hati chafu ni kitendo cha baadhi ya Wakurugenzi kushindwa kusimamia masuala ya fedha na kutelekeza jukumu hilo kwa maafisa wa fedha na kukaimisha Ofisi kila wakato, hivyo kuanzia sasa mkurugenzi yeyote asitoke kwenye kituo chake cha kazi wakati wa vikao vya masuala ya fedha,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Wilaya kutoa taarifa iwapo Mkurugenzi yeyote atatoka katika kituo chake cha kazi wakati wa vikao vya kujadili masuala muhimu ya mipango na bajeti vikiendelea na hasa kwenye vikao vya kamati za fedha pamoja na vya kamati za usalama.

“Katibu Mkuu sitegemei kusikia Mkurugenzi wa Halmashauri anatoka kituoni bila kumpatia taarifa Mkuu wa Wilaya kwani Mkurugenzi anapaswa kushirikiana kiutendaji na Mkuu wa Wilaya, hivyo naamini hilo halitatokea baada ya kikao hiki,” Mhe. Mchengerwa amehimiza.Aidha, Mhe. Mchengerwa amewataka Wakuu wa Wilaya hao kuzingatia mipaka ya madaraka yao kwani wao ni kiungo muhimu cha kuimarisha ushirikiano miongoni mwa viongozi na watendaji wa taasisi zote zilizopo katika ngazi ya wilaya na halmashauri.

“Katika kutekeleza majukumu yenu mnapaswa kuzingatia mipaka yenu ya utendaji kazi na hatua mtakazochukua zizingatie Kanuni, Sheria, Miongozo na Taratibu zilizopo katika Utumishi wa Umma ili mjiepushe na changamoto ya ulevi wa madaraka,” Mhe. Mchengerwa amesisitiza.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.