• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mkurugenzi Mafuru aagiza ujenzi wa 'Government City Complex' ukamilishwe kwa wakati

Imewekwa tarehe: October 24th, 2020

Timu ya menejimenti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma imemuagiza Mkandarasi kampuni ya Mohamedi Builders anayejenga mradi wa jengo la kitegauchumi ‘Government City Complex’ kukamilisha na kukabidhi mradi huo ifikapo tarehe 30 Disemba, 2020.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipoongoza timu yake ya menejimenti kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa kitegauchumi wa jiji ‘Government City Complex’ katika mji wa Serikali eneo la Mtumba jijini hapa.

Mafuru alisema “nimekuja na timu ya Menejimenti ninayoiongoza hapa kumsimamia na kumkumbusha mkandarasi anayejenga mradi huu kuwa kwa mujibu wa mkataba wetu, mradi huu unatakiwa kuisha tarehe 30 Disemba, 2020 na bahati nzuri yeye anasema hana tatizo na kukamilisha mradi huu tarehe hiyo”.

Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa mradi huo umejengwa katika mji wa Serikali yalipo Makao Makuu ya Serikali eneo la Mtumba ili kuwezesha kutoa huduma katika eneo hilo la Mtumba. “Lengo la mradi huu ni kuunga mkono juhudi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakati yeye anapambana kujenga ofisi za Serikali hapa Mtumba, sisi kama Jiji tunapambana kuhakikisha huduma ambazo zitakosekana kwenye maeneo mengine zinapatikana katika jengo hili. Jengo hili lina awamu nne. Hii ni awamu ya kwanza ambayo tumekuja kuishuhudia ikiwa inaelekea ukingoni, nimetaarifiwa kuwa awamu hii ujenzi wake umefikia asilimia 60” alisema Mafuru.

Mkurugenzi huyo aliwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kujitokeza kutembelea mradi huo na kuweka miadi ya kupanga katika jengo hilo. “Mradi huu utakuwa na maeneo ya biashara, ‘apartments’, maduka makubwa ya biashara, sehemu za taasisi za kifedha. Lakini pembeni tunajenga ukumbi mkubwa wa mikutano wenye uwezo wa kuchukua watu 500 ili kurahisisha shughuli zote za Serikali kufanyika katika eneo hili. Eneo hili la mji wa Serikali litakuwa na wageni wengi ambao watakuwa wakihitaji huduma za Serikali, lakini pia mabalozi, wawekezaji na watumishi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi” alisema Mafuru.

Mradi wa ujenzi wa jengo la kitegauchumi la Jiji la Dodoma ulibuniwa na timu ya menejimenti na kupitishwa katika vikao vyake vya kisheria ili utekelezwe na kuiwezesha Halmashauri kuongeza wigo wa mapato ya ndani. Mradi huo, awamu ya kwanza itagharimu shilingi bilioni 18 fedha zinazotoka katika vyanzo vya mapato ya ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Kwa upande wake, Mhandisi Merinyo kutoka kampuni ya Mohamedi Builders alimhakikishia Mkurugenzi wa Jiji kuwa mradi huo utakabidhiwa ifikapo tarehe 30 Disemba, 2020. Alisema kuwa katika kufanikisha kukamilika kwa mradi huo, ujenzi utafanyika usiku na mchana ili kuharakisha mradi huo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru (wa pili kulia) akiongoza timu yake ya Menejimenti kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa "Government City Complex" katika mji wa Serikali Mtumba"

Muonekano wa nyuma wa jengo la kitegauchumi la Jiji la Dodoma "Government City Complex" linalojengwa katika Mji wa Serikali Mtumba.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.