Na Noelina Kimolo.
MKURUGENZI wa Jiji la Dodoma Joseph Mafuru wiki iliyopita amezindua maktaba ya kisasa katika shule ya sekondari Ihumwa mara baada ya kukabidhiwa jengo hilo na taasisi ya Karimjee Jivanjee pamoja na Realising Education for Development ambazo ziliungana na kutengeneza jengo hilo pamoja na kuweka vifaa vya ndani.
Akizungumza katika uzinduzi huo Mkurugenzi huyo alisema anawashukuru na kuwapongeza kwa kuwasaidia katika kukamilisha maktaba hiyo kwani ni kitu muhimu katika kwa wanafunzi pamoja na walimu.
Mkurugenzi Mafuru alisema maktaba inasaidia sana katika kuongeza ujuzi wa mambo mbalimbali kwa kuwa ndani ya maktaba pia kuna vitabu vingine mbalimbali ambavyo vinasaidia katika kuongeza ujuzi zaidi katika maisha.
‘’Maktaba ni kitu cha msingi katika shule inasaidia katika kumuwezesha mwanafunzi kusoma na pia kuweza kutambua vitu vingine tofauti na elimu kama vile bishara kwakuwa katika maktaba pia kuna vitabu vinavyofudisha’’ alisema mafuru.
Mkurugenzi huyo alimpongeza Mkuu wa shule hiyo Mwalimu Greyson Maige kwa ushilikiano mkubwa aliouonesha katika zoezi hilo na kuwasihi walimu wote kuwapa ushilikiano mkuu huyo.
Kwa upande wake Afisa Elimu Sekondari Jiji la Dodoma Upendo Rweyemamu amewashukuru viongozi wa tasisi hizo kwa kuwasaidia katika ukarabati na ununuzi wa vifaa vya maktaba hiyo katika Jiji la Dodoma.
Pia amewasihi walimu wa shule hiyo kusimamia vizuri maktaba hiyo ili iweze kuleta matokeo mazuri ikiwa vita yao daima kuona matokeo mazuri katika shule zote za jiji la Dodoma.
‘’Naomba tuwalipe fadhira kwa kuleta matokeo mazuri vitabu vimeletwa katika wakati ulio sahihi hivyo tuvitumie vitabu hivi katika kubadili matokeo ili maktaba hii ikazae matunda mazuri katika shule yetu’’, alisema Rweyemamu.
Nae mwanafunzi wa shule hiyo Faith Festo amemshukuru mkurugenzi katika uzinduzi wa maktaba hiyo ambayo itawasaidia katika kusoma na kuwafanya wao kufaulu vizuri kwa sababu ndani ya maktaba hiyo kuna vitabu vingi.
‘’Maktaba hii itatusaidia sisi katika kusoma kutokata na vitabu vilivyopo na ninaimani tutafaulu vizuri kutokama na sisi kupata maktaba hii na ninawashukuru wote waliohusika katika kutusaidia kupata maktaba hii’’, alisema Festo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.