WANAFUNZI wa shule ya msingi Ndachi iliyopo katika Kata ya Mnadani jijini Dodoma wametakiwa kusoma kwa bidii ili waweze kufikia ndoto zao na kujiletea maendeleo baada ya kupata elimu hiyo.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipoongoza timu yake ya Menejimenti kutembelea na kukagua ujenzi wa madarasa manne katika shule ya msingi Ndachi na kuzungumza na wanafunzi hao.
Mkurugenzi Mafuru alisema kuwa Halmashauri ya Jiji imeamua kutembelea shule hiyo ili kuona hali halisi. Halmashauri ya Jiji itaendelea kuboresha miundombinu ya shule hii ili kuwawezesha kusoma vizuri katika mazingira bora. “Wajibu wenu ni kusoma kwa bidii na kufaulu vizuri. Elimu ndiyo msingi wa maendeleo hivyo, kupitia elimu mnayoipata shuleni hapa iwasaidie kujiletea maendeleo huko mbele baada ya kumaliza” alisema Mafuru.
Awali Mchumi wa Jiji la Dodoma, Shaban Juma alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ilipeleka shuleni hapo shilingi 61,564,000 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vinne vya madarasa. Alisema kuwa baada ya kupelekwa fedha hizo hali ya ujenzi inaendelea vizuri.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.