MKUTANO wa 27 wa nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi unaendelea katika Jiji la Sharm El Sheikh nchini Misri ambapo kwa wiki ya kwanza viongozi wakuu wa nchi na Serikali wamekutana na kutoa hotuba zao.
Tanzania ni miongoni mwa nchi za Kiafrika zinazoshiriki mkutano huo ambapo Rais Samia Suluhu Hassan aliongoza ujumbe wa Tanzania na kutoa hotuba yake akielezea hatua za Serikali ya Tanzania katika kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Pia, Rais Samia alipata wasaa wa kuzungumza katika moja ya Mikutano iliyoandaliwa na Benki ya Dunia kuhusu miradi mbalimbali ya mazingira inayosaidia kupunguza hewa ukaa.
Aidha, Ofisi ya Makamu wa Rais pamoja na taasisi zingine za Serikali na zisizo za kiserikali zinashiriki katika mkutano katika banda la maonesho la Tanzania ambalo wageni kutoka mataifa mbalimbali wanatembela na kupata elimu kuhusu Tanzania inavyofanya jitihada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
Hotuba za viongozi hao zimejikita katika kuelezea changamoto zinazoikabili dunia kwa sasa ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa athari za mabadiliko ya tabianchi na kutoa mfano wa kuongezeka kwa ukame, joto kali, mafuriko, kupanda kwa kina cha bahari na kuyeyuka kwa barafu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.