Na, Getruda Shomi, DODOMA.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Rosemary Senyamule aipongeza Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kwa kuendelea kutetea haki za binadamu na kuweza kuwafikia watu zaidi ya elfu 3000 katika wiki ya maadhimisho ya Tume hiyo.
Aliyasema hayo alipokuwa akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma katika kilele za maadhimisho ya miaka 20 ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora yaliyofanyika katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center jijini Dodoma.
Senyamule alisema kuwa tume inamchango mkubwa katika kuimarisha utetezi wa haki za binadamu na watanzania, lakini pia imeendelea kuimarika zaidi kadiri siku zinavyozidi kwenda ukulinganisha na hapo awali.
“Tumeshuhudia haki za watanzania zikiimarika na kuwa nzuri kuliko tulikotoka, hiyo ni pamoja na mchango wa Tume hii” alisema Senyamule.
Akitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kwa kutetea haki za watanzania kwa kuimarisha mihimiri ya haki ikiwemo ujenzi wa mahakama na kuongeza watendaji wa kusimamia haki.
“Mheshimiwa Rais ameonesha dhamira ya dhati na uwajibikaji mkubwa katika kutetea haki za watanzania na anatamani kila mtanzania apate haki yake” alisema Senyamule.
Aidha, aliahidi kuwa Mkoa wa Dodoma utaendelea kutoa ushirikiano kwa tume hiyo na vyombo vingine vya haki ili kuhakikisha wanadodoma wanapata haki zao.
“Tutaendelea kutoa kutoa ushirikiano kwa Tume na vyombo vingine ili kuhakikisha nchi yetu na wanadodoma wanapata haki wanayostahili” aliahidi Senyamule.
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora katika maadhimisho yake ya miaka ishirini imepanda miti 600 katika Mkoa wa Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.