MKUU wa Mkoa wa Dodoma , Rosemary Senyamule ameshiriki kufunga mashindano ya Chama cha Netboll Dodoma (CHANEDO) yaliofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma mashindano hayo yaliyoanza tarehe 11 Julai 2023.
Akizungumza na wanamichezo nawananchi walioshiriki katika Mashindano hayo Senyamule amesema michezo ni sehemu ya burudani na inajenga afya hivyo kazi kubwa ni kufanya wengine ambao hawajui na kushiriki michezo waone sababu ya kuipata hii burudani na kujenga Afya kwa ujumla.
Aliwataka washiriki wa michezo hiyo kuwaambia na wengine ili nao mwakani waungane na kuweza kuwahamasisha kuwa miongoni wa timu.
“Niwapongeze timu zote ambazo zimeshiriki katika kuhamasika na michezo hii tushawishi na wengine watumie fursa hii ya michezo wa netiboli kuja kushiriki na kukuza vipaji.
“Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kiongozi mwenye maono makubwa kwa nchi yetu na anatamani Tanzania tufanye vizuri Kwenye sekta ya michezo”Alisema Senyamule.
Dodoma tunataka utalii wa michezo kama Mkoa tumeamua kukuza kila sekta moja wapo hii ya michezo nyie mlioanza ni lazima tuendeleze vipaji hivi ili visiishie kushiriki mwaka huu tu na mwakani tuwashawishi timu nyingi zaidi
Kwa upande wake Mjumbe wa Kamati Tendaji ya Chama cha netiboli Dodoma Mwajuma Mussa Mwinjuma amesema Mashindano ya CHANEDO CUP yamekuwa yakifanyika kila mwaka tangu kuanzishwa miaka 7 iliyopita na Timu zilizoshiriki katika mashindano ni Tisa timu za wasichana 7 na timu za wavulana 2 ikiwa ni pamoja na Afya Zanzibar, The Talents Zanzibar, Benjamin Mkapa hospital Dodoma, Mapindunzi Dodoma, Tanroads Dodoma, Tamisemi, Muungano, Jeshi star na Tume ya Maendeleo na Ushirika Tanzania, alisema Mwinjuma
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.