MKUU wa wilaya ya Dodoma Mheshimiwa Christine Mndeme amekubali jukumu la kuwa mlezi wa vikundi mbalimbali vya usafi na utunzaji wa Mazingira vilivyopo katika Manispaa ya Dodoma, hatua ambayo pia itamuweka karibu zaidi na vikundi hivyo katika kazi muhimu ya kuuweka mji huo katika hali ya usafi na kuvutia ikizingatiwa kuwa ndio Makao Makuu ya Nchi na tayari Serikali imeshahamia mjini humo.
Mheshimiwa Mndeme alitangaza hatua hiyo wakati wa maadhimisho ya kilele cha Siku ya Mazingira Duniani Juni 5 mwaka huu kwa ngazi ya Wilaya yaliyofanyika katika viunga vya Bustani ya Nyerere Square mjini Dodoma.
Katika sherehe hizo, Mkuu huyo wa Wilaya pia alikagua mabanda ya wadau wa utunzaji wa Mazingira na kugawa vifaa mbalimbali vya kufanyia usafi kwa vikundi nane vya usafi vyenye thamani ya shilingi milioni 4.
Sherehe hizo zilihudhuriwa pia na Naibu Meya wa Manispaa ya Dodoma Jumanne Ngede, Ofisa Mazingira wa Manispaa hiyo Dickson Kimari amabaye alimuwakilisha pia Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi, Ofisa Mazingira kutoka Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais Timotheo Mande pamoja na wadau wengine.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.