WANANCHI wanaofanya ujenzi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma wamekumbushwa kuhakikisha majengo wanayojenga yanafuata michoro ya ramani iliyoidhinishwa na Jiji la Dodoma.
Ushauri huo umetolewa leo na Kaimu Mwenyekiti wa Timu Namba mbili ya Menejimenti ya Jiji la Dodoma Joseph Fungo iliyopita katika maeneo ya Swaswa na Ilazo Extention kufuatilia utekelezaji wa masharti ya ujenzi na kudhibiti ujenzi holela katika Jiji la Dodoma.
Fungo amesema kuwa ramani zinazopitishwa na Jiji la Dodoma zinakuwa zimekidhi masharti na vigezo na hivyo kuthibitishwa kuwa zinafaa kujengwa katika Jiji la Dodoma. "Katika ziara yetu tumegundua wako baadhi ya watu wana ramani zilizopitishwa na Jiji lakini majengo wanayojenga yako tofauti na ramani zilizopitishwa na Jiji, utaratibu ni kwamba kila mtu anatakiwa kujenga kama ramani iliyopitishwa inavyoonesha." amesisitiza Fungo.
Naye Mdhibiti wa Ujenzi holela wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Mhandisi Ally Bella amesema yeye na timu yake wataendelea kutekeleza majukumu yao kuhakikisha ujenzi ndani ya Jiji la Dodoma unafanyika kwa maelekezo ya michoro iliyopitishwa. Aidha, amewata watu wote wanaofanya ujenzi jijini Dodoma kuhakikisha kunakuwa na vibali vya ujenzi kwenye maeneo ya ujenzi (site).
"Tumejiandaa na kumejipanga kuhakikisha zoezi la udhibiti wa ujenzi holela hapa jijini linafanyika kwa mafanikio. Ukiacha Watendaji wa Kata, tunao watumishi wa Jiji ambao tumewagawa kwa kanda na jukumu lao ni kutembelea maeneo yao ili kuona shughuli za ujenzi zinazoendelea na kudhibiti ujenzi holela" alifafanua Mhandisi Bella.
Timu Namba mbili ya Menejimenti ya Jiji la Dodoma ikitembelea eneo la Ilazo Extension kudhibiti ujenzi holela jijini Dodoma.
Kaimu Mwenyekiti wa Timu namba mbili ya Menejimenti Joseph Fungo (kulia), Mkuu wa Udhibiti ujenzi holela wa Jiji la Dodoma Mhandisi Ally Bella (katikati) na mdhibiti ujenzi holela Abel Magehema (kushoto) wakiangalia ramani kuona kama ujenzi wa nyumba unaendana na ramani iliyopitishwa na Jiji.
Moja na ujenzi usiokidhi vigezo ambapo timu namba mbili ya menejimenti ilimtaka mwenye ujenzi huo kubomoa mara moja. Pichani askari wa Jiji akiweka agizo la kubomoa.
Hawa walikutwa wakijenga jengo ambalo haliko kwenye ramani na pia limeunganishwa kwenye uzio kitu ambacho ni kinyume na masharti ya ujenzi.
Timu namba mbili ya Menejimenti ya Jiji ikikagua ili kudhibiti ujenzi holela.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.