• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

MOI kuanza upasuaji bila kufungua fuvu

Imewekwa tarehe: January 17th, 2020

Taasisi yaTiba ya Mifupa (Muhimbili Orthopaedic Institute - MOI) inatarajia kuanza upasuaji wa ubongo bila kufungua fuvu mwezi ujao.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Respicious Boniface, wakati akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya taasisi hiyo katika ziara ya maofisa mawasiliano wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, walipoitembelea taasisi hiyo kuangalia mafanikio hayo jijini Dar es Salaam.

Imeelezwa kuwa katika kutekeleza mpango huo, serikali ilitoa Sh. bilioni 7.9 kwa ajili ya kujenga maabara ya kisasa ya upasuaji wa ubongo itakayokuwa na mashine yenye uwezo wa kutibu damu iliyoganda kwenye mishipa ya damu miguuni.

Dkt. Boniface alisema kuwapo kwa maabara hiyo kutaifanya Tanzania kuwa moja ya nchi chache barani Afrika zinazotoa huduma hiyo.

"Mwezi Mei mwaka jana, serikali ilitoa Sh. bilioni 7.9 ili kujenga maabara hii ya kisasa, itakayosaidia upasuaji wa mishipa ya damu katika ubongo.

"Kwa sasa, tunafanya upasuaji kwa kufungua ubongo, lakini kuanzia Februari 15 mwaka huu, tutaanza kufunga mashine hizi za kisasa na kutoa huduma hii kwa njia ya kisasa," alisema.

Dkt. Boniface aliongeza kuwa watafanya upasuaji huo kwa kupitisha vifaa kwenye mishipa ya damu na kuingia kwenye ubongo moja kwa moja na kutibu tatizo kwa muda mfupi na kwa haraka.

Mkuu wa Kitengo cha Radiolojia wa MOI, Dkt. Mechris Mango, alisema mitambo ya kisasa ya kutoa huduma katika maabara hiyo imeshawasili nchini na wanasubiri kukamilika kwa ujenzi wa chumba maalum cha kuifunga ili kuanza kutoa huduma hiyo.

Dk. Mango alisema kuwapo kwa maabara hiyo kutasaidia kupunguza rufani za kwenda nje ya nchi kupata matibabu hayo.

Alisema watakaopatiwa matibabu ni wagonjwa wenye uvimbe wa mishipa ya damu kichwani ili kusaidia kutambua ni mshipa upi unapaswa kufungwa ili kuondoa uvimbe.

Awali, Dkt. Boniface akizungumzia mafanikio ya miaka minne ya uongozi wa Rais John Magufuli katika taasisi hiyo, alisema kuwapo kwa miundombinu ya kisasa kumesaidia kuongeza wagonjwa wa upasuaji kutoka 500 kwa mwezi hadi 900 kwa mwezi.

Alibainisha kuwa jumla ya wagonjwa 43,200 wamefanyiwa upasuaji mbalimbali katika taasisi hiyo, ukiwamo upasuaji wa nyonga 900, magoti 870, mfupa wa kiuno 618, ubongo 880 na watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi 2,070.

Dkt. Boniface alisema gharama za matibabu hayo ndani ya nchi zilikuwa Sh. bilioni 16.5 na kama wangetibiwa nje ya nchi wangetumia Sh. bilioni 54.9, hivyo wamesaidia kuokoa Sh. bilioni 38.4.

Pia, alisema wamefanikiwa kuanzisha huduma za upasuaji wa magoti na mabega kwa njia ya matundu na wagonjwa 800.

Alitaja mafanikio mengine kuwa ni kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu kwenye ubongo kwa wagonjwa watano, kunyoosha vibiongo kwa watoto 12 na upasuaji wa uti wa mgongo kwa kupitia tundu dogo kwa wagonjwa 120.

Alisema katika kipindi hicho wameanzisha wodi maalum ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku hiyo hiyo na wagonjwa 335 wamehudumiwa na huduma ya dawa za usingizi pasipo kulala na wagonjwa 250 walinufaika na hivyo kuwezesha huduma muhimu za matibabu kutolewa nchini kwa asilimia 95.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.