Na. Leah Mabalwe, NALA
Ujenzi wa mradi wa Maji Nala unaotekelezwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA) kwa gharama ya shilingi bilioni 1.3 kutatua changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Kata ya Nala.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Nala, Herman Masila alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliotembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Kata ya Nala.
“Nichukue nafasi hii kuishukuru serikali kutuletea mradi wa maji katika Kata ya Nala. Mradi huu utasaidia sana wananchi kuondokana na adha ya maji. Mradi huu ni mkubwa utasaidia maeneo mbalimbali katika kata yetu inayokuwa kwa kiasi. Kwa siku za usoni tumeshuhudia idadi kuwa ya watu wanakuja kujenga makazi na viwanda. Hivyo, mradi huu utakapo kamilika utasaidia kwa kiasi kikubwa na kupunguza adha ya maji” alisema Masila.
Nae, Mary Kaka ambae ni mkazi wa Kata ya Nala aliipongeza serikali ya awamu ya sita kwa kuendelea kupeleka maendeleo katika Kata ya Nala na kumshukuru rais kwa kuwajengea mradi wa maji kwasababu utawasaidia kutokana na ukosefu wa maji.
“Tulikuwa tunapata shida sana kwasababu ya ukosefu wa maji, tulikuwa tukitoka sehemu ya mbali na kufuata maji sehemu nyingine. Lakini ninaamini mradi huu wa maji utakapokamilika usumbufu na ukosefu wa maji katika kata yetu utapotea kabisa” alisema Kaka.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.