Na. Josephina Kayugwa, DODOMA
MRATIBU wa Mfuko wa Kunusuru Kaya Masikini (TASAF) wa Jiji la Dodoma, Sekunda Kasese amemshukuru Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru kwa kuwaunga mkono kuhakikisha fedha zinawafikia walengwa katika mitaa husika.
Shukrani hizo amezitoa leo tarehe 15 Novemba, 2022 alipotembelewa ofisini kwake na maafisa habari wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwaajili yakupata taarifa ya mfuko wa kunusuru kaya masikini (TASAF).
Amesema katika kipindi cha Septemba hadi Oktoba 2020 TASAF Dodoma imepokea kiasi cha Shilingi milioni 261,835,350 kwaajili ya walengwa 8,017 katika mitaa 222 ambapo wanufaika 2,022 wanapokea fedha kupitia mawakala wa mitandao ya simu.
“Baada ya wanufaika wote kupokea fedha, hupewa fomu za kujaza ili kuthibitisha kama wamepokea fedha hizo, lakini pia tumepokea ambazo kila mtaa utapata Shilingi100,000 kwaajili ya kuwalipa watendaji, wajumbe na wenyeviti wa mitaa na fedha inayobaki itatumika kufanya maboresho ya ofisi,” alisema Kasese.
Mratibu Kasese amesema wajumbe wa Kamati za Mpango za Jamii (CMC) wamerejeshwa kwa lengo la kushughulikia masuala mbalimbali ya walengwa kwenye mitaa kulingana na miongozo ya Mpango wa Kunusuru Kaya masikini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.