Wanachi wametakiwa kuwachunguza na kuwajua wagombea wa ngazi mbalimbali za uongozi ili wasije kufanya makosa katika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani Octoba 2020.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Tume ya Uchaguzi Tanzania, Mroki Mroki katika maonesho ya Nanenane kanda ya kati yanayofanyika Mkoani Dodoma.
Mroki amesema kuwa ni vyema Wananchi wakafahamu vitu vingi kuelekea uchaguzi mkuu ikiwa ni pamoja na kuzitambua sifa za wagombea ambao watawaletea maendeleo katika jamii zao na Taifa kwa ujumla, sifa ambazo watazipata pindi watakapo tembelea katika banda la Tume hiyo lililopo kwenye maoneso ya Nanenane Nzuguni Jijini Dodoma.
“Kubwa zaidi ambalo tume ya uchaguzi tumekuja nalo katika maonesho haya ni hamasa hasa kwa wananchi wa Mikoa hii ya Kanda ya kati, wajitokeze kwa wingi siku ya kupiga Kura lakini kabla ya siku hiyo ni vyema wakazifahamu sifa za wagombea ili wasifanye makosa ya kuwachagua viongozi ambao hawatawasaidia, kwa hiyo wakifika hapa tutawapatia vipeperushi ambavyo vinaelezea sifa hizo.” Alisema Mroki.
Aidha amesema mchakato wa kuchukua fomu kwa wagombea wa Urais umekwishaanza na tayari wagombea wa ngazi hiyo wa vyama vinne vya Siasa wameshachukua fomu hizo.
“Agosti tano pazia la kuchukua fomu za ugombea Urais lilifunguliwa na Tume ya Uchaguzi na sasa hivi vyama vinne vimechukua fomu hizo, ambavyo ni Chama cha Wakulima, NRA, DP na Chama cha Mapinduzi.” Aliongeza Mroki.
Maonesho ya Nanenane yanafanyika kitaifa Mkoani Simiyu ambapo Kanda ya kati yanafanyika Mkoani Dodoma katika viwanja vya Nanenane yenye kauli mbiu inayosema “Kwa maendeleo ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Chagua viongozi bora 2020”.
Afisa Habari wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mroki Mroki akionesha moja na nakala zenye taarifa mbalimbali zinazohusu elimu kwa mpiga kura kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2020.
Wananchi wakipata elimu kuhusu uchaguzi katka banda la Tume ya Taifa ya Uchaguzi katika maonesha ya Nanenane Nzuguni jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.