NAIBU KATIBU mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa Dr. Charles Msonde amesema Msingi wa maendeleo ya Nchi yetu umebebwa na walimu kwani wao ndio kiwanda kikuu cha kuzalisha wataalam mbali mbali na ili waweze kukua na kusimama katika majukumu ya kimaendeleo, mwalimu anajukumu kubwa la kufanya.
Dkt. Msonde amesema hayo katika kikao cha kiutendaji kilichowakutanisha walimu wa shule za Msingi na sekondari, Maafisa Elimu wa Msingi na Sekondari wa Jiji la Dodoma, Maafisa wa Tume ya walimu (TSC) na viongozi kutoka ofisi ya Rais TAMISEMI kilichofanyika katika ukumbi wa shule ya msingi ya St. Gasper.
“licha ya jukumu kubwa la kulea, mwalimu ndiye anayefanya kazi kubwa na nzuri ya mhimu ya kuleta na kumwezesha mtoto apate ujuzi, umahiri, stadi, maarifa na mwelekeo ambao atautumia mtoto kujiletea maendeleo yeye mwenyewe, jamii yake na Taifa kwa ujumla” Dkt. Msonde
Aidha Dkt Msonde serikali inatambua changamoto kuu 6 zinazowakumba walimu wengi nchini ikiwa ni Pamoja na kupandishwa madaraja, kubadilishiwa muundo, mshahara wa Daraja jipya kuchelewa kubadilishwa na malimbikizi ya mishahara kuchukua muda mrefu kulipwa (Salary Arreas), fedha za uhamisho hazitoki kwa wakati, fedha za likizo, Pamoja na kutothaminiwa pale wanawasilisha changamoto zao kwa viongozi, ambapo amesema tayari serikali imeanza kutatua changamoto hizi.
Dkt. Msonde pia amewataka walimu kubadilisha mtazamo wao dhidi ya wanafunzi wanaofanya vibaya Darasani na kuwa na mtazamo Chanya kuwa wanaweza kufanya vizuri endapo wakiamua kuwashika mkono na kuwafundisha vyema.
Akitoa neno la shukrani kwaniaba ya walimu wote walio hudhuria Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Amani Mwl. Job Mwakalambo ameushukuru uongozi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kuahidi kuwa Walimu wataendelea kutekeleza majukumu yao ili kuunga mkono jitihada za Serikali ili kuboresha Taaluma kwa wanafunzi .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.