MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru amewatahadharisha wananchi wanaonunua maeneo na viwanja kiholela jijini Dodoma kuacha mara moja tabia iyo kwani jiji lote lina Mpango wa Matumizi (Master Plan) wa miaka 20 ijayo.
Mafuru alitoa tahadhari hiyo katika kikao cha Baraza la Madiwani wakati akijibu swali la Diwani wa kata ya Mbabala Mhe. Paskazia Mayala juu ya uuzaji wa ardhi holela unaofanywa katika eneo la Chikoa.
Alitoa wito kwa wote wanaohitaji kumiliki kiwanja katika Jiji la Dodoma kuwasiliana na Halmashauri ya Jiji ambayo ndiyo mamlaka inayohusika ili awe na uhakika na kiwanja atakachonunua.
“Dodoma Jiji tuna Mpango Kabambe wa miaka 20 ijayo, unaweza ukanunua eneo huko mtaani kwa madalali ukauziwa eneo la msitu au makaburi, sisi Halmashauri tutakuumbua tu kwa sababu tayari mji mzima wa Dodoma umepangwa” alisema Mkurugenzi huyo.
Baraza hilo lilikutana kwa mara ya pili tangu kumalizika kwa uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani mwishoni mwa mwaka jana.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akijibu hoja za Waheshimiwa Madiwani wa Jiji la Dodoma.
Mhe. Pascazia Mayala Diwani wa Kata ya Mbabala.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.