NAIBU Karibu Mkuu Wizara ya Tamisemi anaeyeshughulikia Elimu Dkt. Charles Msonde amewataka walimu kutumia moja ya Kanuni za kuchunguza uwezo wa mwanafunzi na kutumia nyezo zitakazomwezesha mwanafunzi huyo kuelewa vizuri masomo badala ya kuharakisha kumaliza mada (Topics).
Dkt. Msonde amesema hayo wakati akizungumza na walimu wa shule mbalimbali za Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, amesema ni heri mwanafunzi akafundishwa na kuelewa vizuri hata mada (Topics) 15 kuliko kumharakisha kufundisha ili umalize mada (Topics) 20 na mwanafunzi kutoelewa itakuwa ni kazi bure.
Kwa upande mwingine Dkt. Msonde amewaomba walimu kuendelea kujivunia kuwa katika fani ya ualimu kwakuwa wamepewa kibali cha kumsaidia Mh. Rais Samia Suluhu Hassan katika nyaja ya elimu waendelee kujivunia hilo wakati Serikali ikiendelea kutatua changamoto za malimbikizo ya mishahara,ajira za walimu na maboresho ya madaraja zaidi ya walimu Elfu 54.
Wakati akitoka taarifa ya divisheni ya elimu msingi na sekondari kwa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo Jummane Yassin amesema halmashauri hiyo ina jumla ya shule 103 za msingi na sekondari ambapo idadi ya jumla ya wanafunzi wa shule za msingi ni 90,467 na kwa upande wa shule za sekondari ni 13,502.
Baadhi ya walimu wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe wametoa pongezi zao kwa Naibu Katibu Mkuu Tamisemi Elimu Dkt. Charles Msonde kushuka kuzungumza na walimu hao kwa mifano halisi ya ualimu na kwa hakika kila mmoja aliyesikia atahakikisha watafanyia kazi maelezo yaliyotolewa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.