MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe amemuagiza meneja wa Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kuweka utaratibu mzuri kwa wajasiriamali kufanya shughuli zao kituoni hapo.
Agizo hilo amelitoa leo alfajiri alipofanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho cha mabasi ili kujionea hali ya utoaji huduma, ambapo alisema taswira ya mrundikano wa bidhaa katika eneo la kituo hicho kikuu cha mabasi kilichoanza kutumika hivi karibuni siyo njema.
Akizungumza kituoni hapo, Mstahiki Mwamfupe alisema mrundikano wa bidhaa za wajasiriamali katika maeneo mbalimbali kituoni hapo hasa katika kumbi za abiria kukaa na kusubiri mabasi na bidhaa zilizoenea katika njia zilizotengwa kwa ajili ya abiria kupita ni tatizo.
Akizungumzia hali hiyo, abiria aliyekutwa kituoni hapo Juliana Nyoni alisema kuwa, utaratibu mzuri unatakiwa kuandaliwa ili kuwawezesha abiria kutobughudhiwa na kulinda usalama wao na kwamba utaratibu huo uende sambamba na wafanyabiashara wadogo kufanya biashara zao katika maeneo waliyotengewa ili kutosababisha tafrani.
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma amefanya ziara hiyo katika Kituo Kikuu cha Mabasi Dodoma kujionea hali ya utoaji huduma na kuzungumza na wafanyabiashara na wajasiriamali.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.