MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Anthony Mtaka, katikati ya wiki iliyopita amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia hapa nchini Mhe. Lebius Tangeni Tobius ambapo wamekubaliana kushikiana kwneye maeneno ya Sekta ya Mifugo, Elimu na sekta ya binafsi za Tanzania na Namibia ili kukuza masuala ya uwekezaji na biashara.
Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambapo Viongozi hao wawili wamekubaliana kushirikiana kwenye eneo la mifugo hususani uongezaji tija ya uzalishaji mifugo (ng’ombe) na uongezaji thamani wa mazao ya mifugo ikiwemo nyama, maziwa na Ngozi kwa kuzingatia uzoefu walioanao Namibia katika sekata ya mifugo na fursa kubwa iliyopo Mkoani Dodoma kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo.
Viongozi hao wawili wamekubalia na kukuza ushirikiano katik a seka t elimu ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mtaka amemueleza Balozi Tobius kuwa uboreshaji wa hali ya eLimu ni kipaumbele chake namba moja Mkoani Dodoma na kwamba Dodoma ina fursa kubwa kwa kuwa na Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho ni kikubwa Afrika Mashariki, hivyo kwa kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Namibia wataanzisha programu za kubadilishana wanafunzi na wataalamu mbalimbali wa vyuo ili kubadilishana uzoefu na utaalamu.
Katika kukuza uwekezaji na biashara, Mhe. Mtaka na Balozi Tobius wamekubaliana kuimarisha mahusiano na mashirikiano kati ya sekta binafsi ya Namibia na Tanzania hususani katika Mkoa wa Dodoma, ambapo wamekubaliana kuandaa kongamano litakalofanyika Mkoani Dodoma likihusisha sekta binafsi za pande hizo mbili na maonesho ya bidhaa zinazozalishwa na pande hizo mbli ili kuona maeneo wanayaoweza kushirikiana kwa pamoja.
Mhe. Mtaka alitumia fursa hiyo ya mazungumzo na Balozi Tobius kumualika kutembelea vivutio vya utalii vilivyopo nchini Tanzania vyenye sifa za kipekee Duniani kama vile Mlima Kilimanjaro, Hifadhi za Taifa za Seringeti na Ruaha ili kupitia yeye awaalike watalii kutoka Namibia kuja Tanzania.
Katika hatua nyingine viongozi hao wawili wamekubaliana kuanzisha mahusiano ya kindugu ya mikoa miwili ya Omusati nchini Namibia na Dodoma nchini Tanzania kwa kutambua kuwa Mkoa wa Omusati una sifa na historia ya kipekee kwa kuwa ndio Mkoa ambao Chana cha Ukomboazi wa Namibia cha SWAPO kilizaliwa huku Dodoma ikiwa ni Makao Mkuu ya Tanzania, Chama Tawala cha CCM na Serikali imehamishia shughuli zake hapa Dodoma.
Kwa mujibu wa Viongozi hao wawili, mahusiano kati ya Mkoa wa Omusati Namibia na Dodoma Tanzania yanaendeleza ushirikiano wa undugu wa kihistoria uliokuwepo baina ya Tanzania na Namibia tangu enzi za ukombozi wa Nchi za Kusini wa Bara la Afrika ambapo Tanzania ilichangia kwa kiasi kikubwa katika harakati hizo za ukombozi na kuwa viongozi wengi wa harakati za ukombazi wa nchi za Kusini mwa Afrika waliishi na kupata mafunzo hapa nchini Tanzania.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.