OR - TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa amesema hadi kufikia Machi, 2024 urefu wa barabara za changarawe umeongezeka kwa asilimia 17.45 wakati za lami zikiongezeka kwa asilimia nne.
Mchengerwa ameyasema hayo alipokuwa akielezea utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/23 wakati wa kuwasilisha bungeni makadirio ya mapato na matumizi kwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI na taasisi zake kwa mwaka 2024/25.
Amesema barabara za changarawe umeongezeka kutoka kilomita 24,493 hadi kilomita 41,107.52 sawa na ongezeko la asilimia 17.45 ya lengo huku urefu wa barabara za vijijini na mijini zilizojengwa kwa kiwango cha lami umeongezeka kutoka kilomita 2,025 hadi kilomita 3,224.12 sawa na ongezeko la asilimia nne ya lengo.
“Ofisi ya Rais-TAMISEMI kupitia Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini itaendelea kufanya tafiti kwa kutekeleza kazi za ujenzi wa miundombinu ya barabara kwa kutumia teknolojia mbadala ambapo barabara nne zimeendelea kufanyiwa tafiti ili kupunguza gharama za ujenzi, matengenezo na ukarabati.
Ofisi ya Rais – TAMISEMI kupitia TARURA itaendelea na uboreshaji wa miundombinu ya barabara za vijijini na mijini ili kuwawezesha wananchi kutekeleza shughuli zao za kijamii na kiuchumi ambapo kwa mwaka 2023/24 sekta ya miundombinu ya barabara na usafirishaji iliidhinishiwa Sh bilioni 825.09 kwa ajili ya ujenzi, ukarabati, matengenezo ya barabara na usafirishaji kupitia Mfuko wa Barabara, tozo ya mafuta, Mfuko Mkuu wa Serikali na washirika wa maendeleo.
Amesema hadi Machi, 2024 Sh bilioni 682.60 zimetolewa kwa ajili ya miundombinu ya barabara na usafirishaji, sawa na asilimia 82.73 ya fedha zilizoidhinishwa, ongezeko ambalo limewezesha kujenga barabara za lami kilomita 1,216.65, barabara za changarawe kilomita 17,125.2 na madaraja 2,355.
Mchengerwa amesema kutokana na ongezeko la fedha, kazi zimeongezeka ambapo makandarasi wa ndani wamenufaika na ongezeko hilo la fedha, hivyo wastani wa mikataba 844 ya kazi za barabara imeongezeka na kufikia wastani wa mikataba 1,826
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.