JUMLA ya wanafunzi watahiniwa 10,666 wanatarajiwa kufanya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wote wakitarajiwa kufaulu mtihani huo.
Kauli hiyo iliyolewa na Afisa Elimu msingi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwalimu Joseph Mabeyo ofisini kwake jana jioni alipokuwa akiongelea maandalizi ya wanafunzi hao kuelekea mitihani hiyo inayoanza mapema kesho.
Mwl. Mabeyo alisema kuwa wanafunzi waliosajiliwa kufanya mtihani wa Taifa mwaka 2019 ni 10,666. Kati ya wanafunzi hao, wavulana ni 4,968 na wasichana ni 5,698. Wanafunzi wote waliosajiliwa watafanya mtihani huo kwa mujibu wa ratiba ilivyopangwa.
Akiongelea maadalizi ya wanafunzi kwa ajili ya mtihani huo, alisema kuwa maandalizi yanaenda vizuri. “Maandalizi ya kuwaandaa wanafunzi wahitimu yalianza tangu mwezi Disemba mwaka 2018 ambapo wanafunzi wa darasa la sita hawakufunga na walimu waliendelea kufundisha. Tumekuwa na mitihani ya majaribio ya ndani ya shule na katika Wilaya na ngazi ya Mkoa” alisema Mwl Mabeyo. Akiongelea mtihani wa pamoja uliofanyika mwezi Julai, 2019 baina ya Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Kinondoni, ufaulu ulikuwa asilimia 75.
Mtihani wa kumaliza elimu ya msingi unafanyika tarehe 11-12/09/2019 wakati Halmashauri ya Jiji la Dodoma ikiwa na jumla ya shule za msingi 114, kati ya shule hizo, 93 zinamilikiwa na serikali na shule 21 zinamilikiwa na watu na taaasisi binafsi.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.