RAIS wa taifa jirani la Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni ameipongeza Tanzania kwa kukua kiuchumi na kufikia uchumi wa kati, aidha Rais Museveni ametoa sababu kwa nini ametoa pongezi hizo kwa Watanzania.
Museveni aliyasema hayo jana wakati alipokuwa akitoa salamu mara baada ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kuapishwa kuiongoza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa muhula wa pili wa awamu ya tano kwenye hafla iliyofanyika Jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri.
"...nataka kuwapongeza Watanzania, miezi michache nyuma ilitangazwa kwamba Tanzania kiuchumi imeingia kwenye uchumi wa kati. Nawapongeza kwa sababu mmetuwahi kidogo lakini na sisi tuko tunakuja". Alisema Rais Museveni huku mwenyeji wake Rais Dkt. John Magufuli, Watanzania waliokuwepo uwanjani hapo na wengine waliokuwa wakifuatilia kwenye vyombo vya habari wakionekana kufurahia pongezi hizo.
Vile vile, Rais Museveni alisisitiza kuwa ushiriki wa nchi mbalimbali za Afrika katika sherehe hiyo ni matunda ya msimamo thabiti wa Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na baadhi ya viongozi wa Afrika ambao hawakukubali kuwa vibaraka wa mataifa ya nje.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.