• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mwanafunzi fukara afanya maajabu matokeo kidato cha 4

Imewekwa tarehe: January 11th, 2020

CHANGAMOTO ya mazingira na ufukara wa familia, haukumzuia kijana Yohana Lameck Lugedenga kufaulu vizuri kidato cha nne kutoka Shule ya Sekondari ya Kata ya Igaganulwa mkoani Simiyu. Tukio hili limedhihirisha umuhimu mkubwa wa mpango wa elimu bure ulioanzishwa na Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Magufuli.

Kijana huyo amepata daraja la kwanza, akiwa na ufaulu wa alama A kwenye masomo yote saba, aliyofanya yakiwemo ya Sayansi. Akizungumza kuhusu ufaulu huo, uliowafurahisha walimu wa shule hiyo pamoja na uongozi wa Mkoa wa Simiyu, Mkuu wa Shule hiyo, Emelius Emmanuel alisema walitarajia matokeo mazuri kwa Yohana, ingawa sio kwa kiwango hicho.

“Kwa kweli tuliona uwezo wake tangu akiwa kidato cha kwanza, tulitegemea angepata daraja la kwanza ila sio kwa alama zote hizo, lakini ametushangaza na sisi tumefurahi kupita maelezo, hasa ukizingatia ufukara wa familia yake”, alisema Mwalimu Emmanuel.

Alisema Shule ya Sekondari Igaganulwa ni ya Kata na kwenye matokeo ya kidato cha nne yaliyotoka juzi, wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 88, na waliofaulu ni 75 ambao wamepata kuanzia daraja la kwanza hadi la nne na wengine 13 wamefeli.

Shule hiyo ya Sekondari Igaganulwa, ipo umbali wa takribani kilometa 45 kutoka Bariadi mjini. Akizungumzia ufaulu wa Yohana, ambaye ndiye mwanafunzi pekee aliyepata daraja la kwanza tena kwa alama A za masomo yote saba, Mwalimu Emmanuel alisema siri ya ufaulu huo ni juhudi binafsi na makambi ya masomo, yanayofanywa mkoani humo.

“Yohana ni mtoto mtaratibu, alistahili ufaulu huo, ametoka mazingira magumu mno, anaishi na mama pekee, baba yao aliondoka nyumbani mwaka 2013 akidai anakwenda kutafuta maisha mkoani Morogoro, ila hadi leo hajarejea na hana mawasiliano na familia yake”, alisema Mwalimu Emmanuel.

Akisimulia aliyopitia Yohana, Mwalimu Emmanuel alisema baada ya kufaulu elimu ya msingi na kujiunga na Sekondari ya Igaganulwa, mtoto huyo alichelewa kuripoti shuleni hapo.

Walimu hawakujua tatizo lake hadi pale walimu wa shule ya msingi aliyosoma, walipowaambia kuwa anakabiliwa na matatizo ya kifamilia. Mwalimu Emmanuel alisema walimu hao wa msingi, ndio waliwaambia walimu wa Sekondari ya Igaganulwa kuwa hata sare za shule, walikuwa wakimnunulia na vifaa vingine. Waliomba asaidiwe sekondari, kwa kuwa ana uwezo kimasomo.

“Aliripoti shuleni kwa kuchelewa, kwa sababu mama yake alikuwa hana uwezo hata wa kumnunulia sare, tulimsaidia sare za shule, akaanza masomo na uwezo wake ukaanza kuonekana. Tuliona sio busara kumuacha, tukamsaidia. Na mimi ni mwalimu wa Hesabu, alikuwa kinara, na anajua kudadisi na ana nidhamu ya hali ya juu’’, alifafanua zaidi Mwalimu Emmanuel.

Mwalimu huyo aliongeza kuwa walipofanya mtihani wa kidato cha pili, aliibuka na matokeo mazuri. Pia mtihani wa majaribio wa kidato cha nne alifanya vizuri, na hiyo ikamfanya aende kambi mkoani, ambapo walimu walimsaidia gharama, na mama yake mzazi, alipeleka debe moja la mahindi.

“Huwa mkoa umeweka utaratibu wa kuinua kiwango cha elimu kwa kuanzisha makambi ya masomo na huyo kijana alichaguliwa kwenda kambi ya masomo mkoani ambako utaratibu wazazi huchangia gharama ndogo. Lakini, kwa Yohana mama yake alishindwa, ila akaleta debe la mahindi na sisi tukachanga na kupata fedha za kujikimu akaenda kuungana na wenzake ili wanolewe zaidi’’, alikazia Mwalimu Emmanuel.

Akizungumzia matokeo hayo, Mwalimu Emmanuel alisema waliposikia ufaulu huo walishangilia, sio kwa sababu Yohana amepata daraja la kwanza pekee, bali kwa sababu amepata masomo yote saba alama A.

“Asubuhi ya leo (jana) Yohana alikuja shuleni hapa, kutoa shukrani kwa walimu kwa kumsaidia na kumtia moyo kusoma kwa bidii, na mwalimu wake wa somo la Kiswahili alikuwa na wasiwasi kwa sababu masomo mengine alikuwa akifaulu kwa alama A lakini Kiswahili akawa anapata B, alimsihi sana kukazania pia somo hilo na kweli leo matokeo yamedhihirisha kwani kapata alama A zote”, alisema.

Kwa mujibu wa Mwalimu Emmanuel, Yohana ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yao kusoma. Kwamba ana mdogo wake wa kike, ambaye ufukara wa familia na mazingira, vimechangia yeye kutokuwa na mwelekeo mzuri.

“Unajua nilienda nyumbani kwao, yaani mazingira yale sio ya kawaida, ni fukara na ninasikia pia hapo sio kwao, bali wamepewa wajihifadhi. Wakati mwingine hata mlo mmoja ni tatizo, ndio maana alipoingia kidato cha nne tulimchukua Yohana akaishi shuleni ili atulie asome” alisema. Yohana amepania kuwa daktari. Akizungumzia furaha ya matokeo yake, Yohana alisema amefurahi sana kupata matokeo hayo.

Kwamba mama yake aliposikia habari hiyo njema, alimshukuru na kumwambia asante. “Kwa kweli nimefurahi kupata matokeo haya, mama aliposikia nimefaulu alinishukuru, alisema asante mwanangu, na mimi naahidi kufanya vizuri nikichaguliwa kidato cha tano, nataka kuendelea na masomo yangu ya Sayansi, ili baadaye nije kuwa daktari, niikomboe familia yangu”, alisema Yohana.

Alisema familia yake ina watoto wanne, mmoja ni marehemu na kwamba yeye pekee ndiye aliyebahatika kufika kidato cha nne, kwani mdogo wake aliishia kidato cha pili na hiyo ilichangiwa na mazingira magumu waliyonayo. Yohana aliiomba serikali impangie shule yenye mazingira mazuri na kumsaidia mahitaji, kwa sababu ufukara wa familia yake, unaweza kuwa kikwazo katika masomo yake, hivyo akipata shule nzuri yenye mazingira bora, atatulia na kusoma.

“Nawashukuru walimu na mama walinisaidia kunishauri na kuniongoza hadi nikafika na kupata matokeo haya. Naiomba serikali isiniache, inisaidie, kama kuna uwezekano nipate shule nzuri na mazingira mazuri nitulie nifanye vizuri zaidi”, aliomba Yohana.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.