MBUNIFU Maleo Lameck (pichani juu) amebuni mashine kwa ajili ya kuwawezesha Watoto wa kike kununua taulo za kike “Sanitary Nepkin Vending Mashine” kwa usiri na gharama nafuu.
Lameck alisema kuwa lengo la ubunifu huo ni kuwasaidia watoto wa kike kuwa wasiri katika masuala ya hedhi. “Bei rahisi kununua pedi kwa sababu ni shilingi 200 kwa pedi moja. Hii inamsaidia mtoto wa kike pale anapoingia kwenye hedhi ghafla. Tofauti na kwenda kununua pedi dukani kwa zaidi ya shilingi 2,000” alisema Lameck.
Mbunifu huyo alibuni mashine hiyo akiwa kidato cha tatu mwaka 2017 katika shule ya sekondari ya Kondo iliyopo mkoani Dar es Salaam.
Akizungumzia gharama ya kutengeneza mashine hiyo, mbunifu huyo alisema kuwa mashine hiyo inagharimu shilingi milioni tatu. “Taarifa ya bajeti imewasilishwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa hatua zaidi” alisema Lameck.
Ikumbukwe kuwa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inaendesha Mashindano ya Kitaifa ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (MAKISATU) kwa madhumuni ya kutambua, kuadhimisha, kujenga, kukuza na kuendeleza ubunifu wa watanzania katika nyanja za sayansi na teknolojia ili kuchangia juhudi za kuifanya Tanzania kuwa na uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanja.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.