Mwanasiasa mkongwe, Balozi Job Lusinde (90) ambaye alikuwa miongoni mwa baraza la kwanza la mawaziri la Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere baada ya uhuru, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumanne, Julai 7, 2020, katika Hospitali ya Mloganzila jijini Dar es Salaam.
Familia ya Lusinde na Malecela imesema taratibu za mazishi zinaendelea katika makazi yake, Kilimani, jijini Dodoma. Balozi Lusinde ni kaka wa Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania, Mzee John Malecela.
Lusinde aliyezaliwa Oktoba 9, 1930, aliwahi kuwa Waziri wa Mawasiliano mwaka 1965 na ni miongoni mwa watu waliofanya kazi kwa ukaribu na Mwalimu Julius Nyerere kama Waziri wa Serikali za Mitaa mwaka 1961. Pia, aliwahi kuwa Balozi wa Tanzania nchini China kuanzia mwaka 1975 hadi mwaka 1984.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.