MAKAMU wa pili wa Rais wa Zanzinbar Mhe. Hemed Suleiman Abdul amezindua rasmi Mbio Maalum za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Kusini Unguja visiwani Zanzibar mahali alipozaliwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan na zitahitimishwa mkoani Geita wilaya ya Chato mahali alipozaliwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa awamu ya tano.
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati akiwasilisha salamu za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mbele ya mgeni rasmi.
“Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni maalum, mtaona zilipozinduliwa ndipo alipozaliwa Mheshimiwa Rais Samia na zitahitimishwa Oktoba 14 Wilayani Chato mahali alipozaliwa hayati Magufuli” amesema Mhagama.
Aidha, katika kuonesha kuwa serikali ya awamu ya sita imeona umuhimu wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika ukuaji wa uchumi na maendeleo ya nchi, Mwenge wa Uhuru wa mwaka huu umebeba kauli mbiu isemayo ‘TEHAMA ni msingi wa Taifa endelevu itumike kwa usahihi na uwajibikaji”.
Amesema lengo la Serikali kupitia ujumbe huu ni kutimiza na kuhakikisha mamlaka zote za Serikali kuanzia ngazi ya chini hadi taifa zinatumia mifumo ya kielekroniki katika kuongeza ufanisi wa kiutendaji hasa katika ukusanyaji wa mapato na utawala wa siku kwa siku wa utendaji kazi ndani ya Serikali. Tukitumia teknolojia hii tunaweza kuongeza ukuaji wa uchumi na kulifanya Taifa kuendelea kwenye uchumi wa kati wa kiwango cha juu.
Naye Kaimu Waziri Wizara ya Habari, Vijana na Michezo, Leila Mohamed Musa amesema Mwenge huo utakimbizwa katika Wilaya 150 za kiutawala badala ya wilaya 195.
Amesema kupitia mbio hizo wananchi watabuni na kuanzisha miradi kwa ajili ya maendeleo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.