• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mwenge wa Uhuru, 2023 wazindua Kituo cha Afya Nkuhungu

Imewekwa tarehe: October 3rd, 2023

Na. Dennis Gondwe, NKUHUNGU

MWENGE wa Uhuru mwaka 2023 umezindua Kituo cha Afya Nkuhungu ili kiweze kuwahudumia watanzania baada ya kujiridhisha na ujenzi wa kituo hicho na nyaraka kufuatia ukaguzi uliofanyika.

Kauli hiyo ilitolewa na Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim alipoongoza Mwenge wa Uhuru kutembelea na kukagua ujenzi wa Kituo cha Afya Nkuhungu kilichopo jijini Dodoma.

Kaim alisema kuwa Mwenge wa Uhuru umepita kwenye Kituo cha Afya Nkuhungu na kusema kuwa ujenzi wake umefanyika vizuri. “Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya pamoja na maelekezo ambayo nimetoa kwa dhati kabisa na kwa heshima ya Mheshimiwa Rais na wananchi hawa niseme Mwenge wa Uhuru mwaka huu tumeridhia uzinduzi wa kituo hiki cha afya” alisema Kaim.

Akisoma taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Afya Nkuhungu kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Mkuu wa Divisheni ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Dkt. Andrew Method alisema kuwa halmashauri inatekeleza mradi huo kupitia mapato ya ndani ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Tamisemi ya kujenga vituo vitatu vya afya kupitia mapato ya ndani. ”Vituo vingine vinavyojengwa kupitia mapato ya ndani ni Zuzu na Kizota ambavyo vipo katika hatua ya umaliziaji. Lengo la mradi huu ni kusogeza huduma za Afya karibu na wananchi wa Kata ya Nkuhungu yenye wakazi 49, 337. Vilevile, kituo hiki kinahudumia wananchi wa kata za jirani za Kizota yenye wakazi 30,632 na Mnadani yenye wakazi 44,311 pamoja na kutoa huduma za rufaa kwa Kata za Chigongwe yenye wakazi 8,933, Nala yenye wakazi 11,715 na Mbalawala yenye wakazi 11,370” alisema Dkt. Method.

Akiongelea mafanikio ya mradi huu aliyataja kuwa ni kuhudumia wakazi 49,337 wa Kata ya Nkuhungu. “Vilevile, wakazi 106,961 wa Kata jirani za Kizota, Mnadani, Chigongwe, Nala na Mbalawala wananufaika na huduma za Afya kupitia kituo hiki. Wajawazito 5,470 na watoto 20,786 wenye umri chini ya miaka mitano wanatarajiwa kunufaika na huduma za Afya ya uzazi na mtoto” alisema Dkt. Method.

Kuhusu gharama za mradi, alisema kuwa hadi kukamilika awamu ya kwanza shilingi 382,996,246 zimetumika zikihusisha ujenzi wa majengo ya kutolea huduma, kichomea taka na ununuzi wa vifaa. “Ujenzi wa majengo shilingi 322,996,246.00 na ununuzi wa vifaa na samani shilingi 60,000,000” alisema.

Ikumbukwe kuwa huduma zinazotolewa baada ya kufunguliwa kwa kituo cha Afya Nkuhungu ni Afya ya uzazi na mtoto (RCH Clinic) kwa wajawazito na watoto wenye umri chini ya miaka mitano, huduma za matibabu ya Wagonjwa wa Nje (OPD) na huduma za Maabara.

Mkazi wa Nkuhungu, Mwaimvua Abdallah alisema kuwa uzinduzi wa kituo hicho cha afya ni ukombozi kwa wanawake waliokuwa wakilazimika kutembea umbali mrefu kufuata huduma za tiba mjini.

         

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.