Mwenge wa Uhuru leo Agosti 5, 2018, umeingia na kuanza mbio zake katika Wilaya ya Dodoma ambapo ulikabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Patrobas Katambi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Simon Ezekiel Odunga katika eneo la Makutupora, ambapo utapitia miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 5.2 inayotekelezwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma, kabla ya kuendelea na mbio hizo katika Wilaya ya Bahi Julai 6, mwaka huu.
Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2018 unakimbizwa na vijana sita wakakamavu wakiongozwa na mkimbiza Mwenge Kitaifa Mhandisi Charles Francis Kabeho.
Baada ya kukabidhiwa kwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Mwenge wa Uhuru ulikimbizwa umbali wa kilometa 81, ambapo umepitia miradi saba na umefanya shughuli za kuweka mawe ya msingi, kuzindua na kutembelea miradi hiyo, huku Miradi yote ikikaguliwa kwa umakini na kukubaliwa kuwa imekidhi viwango na thamani ya pesa.
Miradi iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru ni Mradi wa Matofari na ujenzi katika Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Makutupora, Mradi wa ujenzi wa barabara ya Emmaus-African Dream kwa kiwango cha Lami ikiwa na urefu wa kilometa 1.4, Mradi wa Kituo cha Mafuta cha GP 88 kilichopo Kata ya Dodoma Makulu, na mradi wa Karakana ya Ufundi Seremala katika Chuo cha Ufundi Stadi (VETA).
Miradi mingine iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru kwa mwaka huu ni ujenzi wa Maabara Biolojia na Kemia katika Shule ya Sekondari ya Dodoma, na upanuzi wa kituo cha Afya Makole.
Wakimbiza Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa wakishirikiana na wananchi wa Jiji la Dodoma kukimbiza Mwenge wa Uhuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.