MIRADI mitano yenye thamani zaidi ya shilingi bilioni 3.3 imetembelewa ,kuzinduliwa na kuwekewa jiwe la msingi na Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Dodoma.
Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma , Jabir Shekimweri wakati akiongea na wakazi wa Kata ya Chang’ombe uwanja wa shule ya msingi Chang’ombe kwenye mkesha wa Mwenge wa Uhuru.
Shekimweri alisema “Mwenge wa Uhuru umekimbizwa km 129.5 na kuzungukia miradi mitano ambayo ni mradi wa ujenzi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza iliyopo Mapinduzi East, mradi wa ujenzi wa barabara ya km 1 Kisasa nyumba 300, mradi wa kilimo wa kikundi cha vijana Kiu ya Ufanisi Nanenane, mradi wa ujenzi wa hotel ya Southern Empire na mradi wa kituo cha afya Chang’ombe”.
“Niwaondoe hofu wanachang’ombe, Wilaya ya Dodoma tupo vizuri Mwenge wa Uhuru umezunguka katika miradi mitano kati ya hiyo miradi mitatu imewekewa jiwe la msingi na miradi miwili imezinduliwa changamoto ndogondogo zilizojitokeza tunaahidi kuzirekebisha na ushauri uliotolewa tutaufanyia kazi”.aliongezea Shekimweri
Akizugumza mara baada ya kuzindua miradi na kuweka jiwe la msingi katika miradi kadhaa kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Sahili Geraruma aliwataka watendaji wa Halmashauri kote nchini kuacha kufanya kazi kwa mazoea kuhakikisha miradi inazingatia thamani ya fedha na kuwa katika ubora.
“Mwenge wa Uhuru umepita kwenye miradi mitano ni mizuri tumeridhishwa nayo. Nitoe rai kwa watendaji msitengeneze mazingira ya kuonyesha mmetumia pesa vibaya zingatieni taratibu za matumizi ya pesa, taratibu zifuatwe changamoto ndogondogo zilizojitokeza kwenye mradi wa shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza na mradi wa kituo cha afya Chang’ombe mzifanyie kazi”. alisema Geraruma
Geraruma alimalizia kwa kutoa rai kwa wakazi wa wilaya ya Dodoma kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kujitokeza kuhesabiwa tarehe 23/08/2022 kwa maendeleo ya Taifa zima.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.