Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Dodoma mjini ameendelea na ziara yake ya kutembelea miradi ya maendeleo iliyopo ndani ya jiji la Dodoma akiwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya siasa pamoja na mwenyeji wa ziara hizo Mkuu wa wilaya ya Dodoma mjini Patrobas Katambi.
Ziara hii ni muendelezo wa ziara zinazofanywa na kamati hiyo ya siasa ya wilaya kwa muda wa siku nne, kwa lengo la kukagua na kuhakikisha ilani ya Chama Cha Mapinduzi inatekelezwa kwa usawa na kwa wakati.
Msafara ulianzia katika kituo cha Afya cha Hombolo ambapo Mganga Mfawidhi Mwanadamizi Dkt. Steve Chikoti alitoa ufafanuzi wa pesa walizopewa na Serikali kiasi cha Shilingi million 500 kwa ajili ya ukarabati wa chumba cha kuhifadhia maiti , ujenzi wa maabara , nyumba ya mtumishi, wodi ya wanawake na chumba cha upasuaji.
Aidha, Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma iliwaongezea shilingi million 130 ili kukamilisha ujenzi wa njia za kuunganisha majengo (Korido) na kukarabati majengo ya zamani.
Baadae kamati ilikwenda Mtumba eneo la mji wa serikali kwenye mradi wa kitega uchumi cha Jiji na walioneshwa jinsi mradi unavyoanza na mikakati iliyowekwa kukamilisha miradi hio kwa wakati.
Kamati ilitembelea Shule ya Msingi Ilazo ambako huko Mkuu wa shule Mwalimu Martha Henry Risasi alitoa maelezo jinsi mradi wa ujenzi wa shule hio mpya ambayo imetimiza miaka miwili tu tangu ianzishwe.
Katika ujenzi wa shule hiyo serikali imewekeza zaidi tya million 105 kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na jengo la utawala.
Msafara ulimalizia ziara yake katika shule ya msingi Mnyakongo ambayo imejengwa kwa lengo la kupunguza adha ya wanafunzi wengi wanaosoma shule ya msingi Nkuhungu hali wakiishi mbali . Ilielezwa kuwa shule hiyo sasa imelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi, ina wanafunzi takribani 3,000 hivyo ujenzi wa shule ya Mnyakongo umeleta manufaa makubwa kwa wananchi wa na wanafunzi kwa ujumla.
Mwenyekiti Mwinje alitoa shukrani kwa watekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kuanzia mwenyekiti wa Taifa na Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzanzia Dkt. John Pombe Magufuri hadi kwa mwenyekiti wa mtaa kwa kutekeleza majukumu ya serikali kwa uangarifu mzuri wa mali za umma.
Naye Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi alitaadharisha kuwa “kwa watumishi wengine mnapaswa kuwa wawajibikaji na wachapa kazi kwa umakini wa hari ya juu ili msije kumuangusha Raisi, kwani msipofanya kazi vizuri mimi sitacheka na mtu hata kidogo, kwani mimi kabla sijatumbuliwa wengine wasio wawajibikaji watakuwa pabaya".
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.