SERIKALI imezindua Mwongozo wa Uanzishaji na Uendeshaji wa Dawati la kutokomeza Ukatili wa Kijinsia katika maeneo ya Umma ili kuwasaidia wananchi kwenye maeneo hayo kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Akizindua Mwongozo huo, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, katika soko la Mbuyuni wilayani Moshi, mkoani Kilimanjaro ameitaka Jamii kushirikiana kutokomeza vitendo vya ukatili kupitia Kamati za ulinzi wa Wanawake na watoto kwenye maeneo yao.
Dkt. Gwajima amesema Mwongozo huo ni wa kila mdau ambaye anatekeleza ajenda ya Serikali ngazi zote yaani kuanzia wananchi wenyewe, viongozi wa Serikali ya mtaa au kijiji, watendaji wa Kata na Halmashauri na hata wanasiasa.
"Natarajia kila mdau ataona umuhimu wa kusoma na kutekeleza mpango wa ufuatiliaji ulioelezwa kwenye Mwongozo huu kwani utahusisha taarifa za mikoa kuwasilishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI na kisha Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu ambapo itampelekea Waziri Mkuu ambaye, Ofisi yake ndiyo inaratibu masuala yote ya kisekta ya kupambana kutokomeza Ukatili wa Kijinsia" amesema Dkt. Gwajima.
Aidha, Dkt. Gwajima amehimiza Mwongozo huo kunasambazwa kila mkoa kwa kushirikiana na Wizara katika Ili kuanzisha Madawati hayo katika maeneo ya Umma.
Dkt Gwajima ameongeza kwamba, anatambua Jamii ina vipaumbele vingi ikiwemo Elimu, afya, maji, umeme, Bararara ambavyo vinavyojadiliwa kwenye vikao vya kata na vijiji na kusisitiza kuwa ajenda ya kuwalinda watoto na Wanawake iongezwe pia katika ajenda hiyo iwe ya Kudumu.
Aidha ameishukuru Ofisi ya Rais TAMISEMI kuzielekeza mamlala za Serikali za Mitaa kuweka Sheria ndogo na kufanya ajenda ya ukatili kuwa ya Kudumu kwenye vikao vyote vya maamuzi.
"Tukaisimike ajenda hii kwenye vikao vyote, kutoijadili ni kama kuvibariki vitendo hivi kuendelea" ameongeza Dkt. Gwajima.
Hali kadhalika, Dkt. Gwajima amesisitiza kuwa Mwongozo huo ni sehemu tu ya mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia hivyo wananchi wote washirikiane.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.