WATU 30,000 hufariki kila mwaka nchini kutokana na magonjwa mbalimbali wanayoyapata kwa sababu ya kutumia Nishati chafu ya kupikia ikiwemo kuni na mkaa.
Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais, Christina Mndeme ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ambapo alitembelea Kikosi cha Jeshi 833 Oljoro pamoja na Hospitali ya Mount Meru ambao hutumia nishati safi.
Mndeme amesema kutokana na ukataji miti kwa matumizi ya kuni na mkaa kumekuwa na athari nyingi katika afya kwa mtumiaji hasa mtoto na mwanamke ambaye muda mwingi anakuwa jikoni na mwisho mfumo wake wa upumuaji huathirika.
“Unapotumia nishati chafu, kitaalamu ni sawa na kutumia muda wa saa saba kupika kwa wiki wakati nishati safi ni sawa na saa moja, hivyo nishati safi huokoa muda kwa mtumiaji kupata nafasi ya kufanya vitu vingine,” amesema Mndeme.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Victor Rutayugwa amesema kabla ya kutumia nishati safi walikuwa wakitumia kuni tani 30 kwa mwezi ambapo ilikuwa ikiwagharimu kiasi kikubwa cha fedha.
“Kikosi kilipokea maelekezo ya kuhakikisha inaachana na matumizi ya kuni ikiwa ni mpango wa utunzaji wa mazingira na mwaka 2021 kikosi kilianza kutumia gesi kwa kuweka miundombinu.”
Hata hivyo, Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha Dk. Kipipa Mlambo amesema kiafya matumizi ya kuni na mkaa yalikuwa yakiathiri watu wengi lakini kwa sasa elimu imewasaidi watumiaji wengi na wanaachana na matumizi ya kuni na mkaa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.