Na. Shaban Ally, DODOMA
NAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Emmanuel Chibago ameipongeza Benki ya NMB kwa kutoa vifaa vya kuhifadhia taka 100 vyenye thamani ya shilingi milioni 20 kwa lengo la kuunga mkono Sera ya utunzaji wa mazingira katika jiji hilo na viunga vyake.
Pongezi hizo alizitoa katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kuhifadhia taka lililofanyika katika uwanja wa Nyerere Square jijini hapa jana baina ya NMB na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
"Naomba tuwashukuru sana ndugu zetu wa benki ya NMB kwa jambo hili mlilolifanya. Hakika mmetupunguzia mzigo mkubwa sisi kama halmashauri wa kutafuta fedha kwa ajili ya vifaa vya kutunzia taka" alisema Chibago.
Aidha, aliahidi kuwa halmashauri yake itavitunza vifaa hivyo vya kuhifadhia taka ili viweze kutumika kwa muda mrefu. Alisema kuwa gharama iliyotumika kununulia vifaa hivyo ni kubwa sana, hivyo lazima vitunzwe.
"Mmetuasa habari ya utunzaji wa hivi vifaa naomba tulipokee, tutalitekeleza kwa kulitungia sheria ndogo kwa ajili ya kuwabana watu wanaotumia vifaa hivyo ili wavitunze viwe endelevu" aliongeza Chibago.
Naibu Meya huyo alimshukuru Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, kwa Kupigania upatikanaji wa vifaa vya kuhifadhia taka ili kuimarisha usafi ndani ya jiji hilo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.