NAIBU Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde amefurahishwa na mpango wa mafunzo baina ya Taasisi ya Maafisa Watendaji Wakuu (CEOrt) na Chuo cha Biashara cha Strathmore ambayo yanalenga kuwajengea uwezo Watanzania kushika nafasi za juu katika makampuni mbalimbali na taasisi za Biashara hapa nchini na hivyo kutasaidia kuongeza nguvu kazi yenye sifa na ujuzi stahiki katika uongozi wa makampuni.
Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akipokea tuzo ya heshima ya KIONGOZI WA UMMA ALIYETOA MCHANGO KWA SEKTA BINAFSI 2019 aliyokabidhiwa na CEOrt kutambua mchango wake katika kuwezesha mafunzo kwa ajili ya Watanzania kushika nafasi za juu za uongozi katika makampuni ijulikanayo kama CEO APPRENTICESHIP PROGRAMME (CAP).
"Miaka mitatu iliyopita nilialikwa na Marehemu Ali Mufuruki aliyekuwa Mwenyekiti wa CEOrt, mkaniambia kuhusu kukosekana kwa Watanzania wenye sifa za kuwa Watendaji Wakuu wa Makampuni. Nikawapa changamoto kwamba mshirikiane na serikali kutatua changamoto hiyo. Leo nina furaha kuliona kundi la kwanza la Vijana 16 wakiwa katika mafunzo ya Uongozi wa juu wa makampuni, lengo letu ni kuwezesha Vijana wengi zaidi kupata ujuzi ili kuongeza wigo wa watanzania wenye sifa za kushika nafasi za juu za uongozi wa Makampuni na Taasisi za Biashara" Alisema Mavunde.
Naye Mwenyekiti wa CEOrt Bw. Sanjay Rughan ameshukuru ushirikiano uliopo baina ya Serikali na sekta binafsi, kueleza kwamba wamejipanga kuhakikisha kundi kubwa la Vijana wa Kitanzania wanapata fursa ya mafunzo ili kuondoa tatizo la ukosefu wa watu wenye sifa za uongozi wa juu katika makampuni hapa nchini.
Akishukuru kwa niaba ya wanufaika wa Programu hii, Bw Unguu Ramadhan Sulay, ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Fedha wa Kampuni ya Plasco Ltd, amepongeza wazi la kuja na mafunzo haya ambayo yamewaongezea uelewa mkubwa wa masuala ya Uongozi wa kampuni katika kuwatayarisha kushika nafasi za juu za uongozi na kuahidi kutumia mafunzo hayo vizuri ili kutimiza liliokusudiwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.