NAIBU Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Kangi Lugola ameanza ziara ya kikazi ya wiki moja katika Manispaa ya Dodoma jana ambapo alitembelea Ofisi za Halmashauri na kupokea taarifa ya hali ya Mazingira kwa ujumla iliyowasilishwa na Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu Dickson Kimaro.
Naibu Waziri pia alipata taarifa kutoka kwa wataalam wa taasisi zingine ambazo ni wadau wa Mazingira ikiwemo Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dodoma (DUWASA), Idara ya Madini, na Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambao amefutana nao katika ziara hiyo.
Katika siku ya kwanza ya ziara yake hapo jana, Naibu Waziri Lugola alitembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na Chuo Kikuu cha Mtakatifu John ambapo alikagua mifumo ya usimamizi wa taka ambapo kwa ujumla alikiri kuridhishwa jinsi taasisi hizo zinavyozingatia matakwa ya Sheria na taratibu za kuhifadhi Mazingira, lakini aliziagiza kuhakikisha takataka zinazoteketezwa kwa kuchomwa moto zinateketea kwa kiwango kinachokubalika.
Ziara ya Naibu Waziri inaendelea leo Ijumaa Mei 18, 2018 ambapo pamoja na maeneo mengine, atatembelea na kukagua mifumo ya usimamizi wa taka katika machinjio ya Punda iliyopo eneo la Kizota na inatarajiwa kumalizika Mei 25, mwaka huu.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.