NAIBU WAZIRI wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kufanya mazungumzo na wadau wa sekta ya kilimo kutoka kampuni ya Berga & More ambao wanalengo la kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji hususani katika bonde la Mto Rufiji.
Ujumbe huo ambao ulionogzswa na Dott.ssa Rita Ricciard ambaye ni moja ya waanzilishi wa Kampuni hiyo, umemueleza Mhe. Mavunde kuwa dhamira yao ya kuwekeza imesukumwa na Tanzania kufungua milango ya uwekezaji kwa wawekezaji wa Kimataifa.
“Tayari tunafanya kazi nchini Uganda na Kenya, hivyo tumeona fursa kuwa iliyopo Tanzania na kututiwa sana kwa lengo la kuleta wawekezaji wakubwa kwenye sekta ya umwagiliaji nchini” aliongeza Bi. Dott.ssa.
Vilevile, Mhe. Mavunde aliwaeleza wawekeazaji hao kuwa, Serikali inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imedhamiria kuongeza uwekezaji kwenye umwagiliaji, na sisi kama Wizara yenye dhamana tunawahakikishia kuwa tutafanya yote kwa upande wetu ili kufanikisha uwekezaji huu muhimu.
“Tumejiwekea lengo la kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikapo mwaka 2030, hivyo ni dhahiri kwamba lengo hili hatutaweza kulifikia pasipo kuweka mkazo mkubwa kwenye kuendeleleza miradi ya umwagiliaji, hiki ni kipaumbele chetu namba moja” alibainisha Mhe. Mavunde.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, Bw. Raymond Mndolwa alimwahidi Mhe. Mavunde kuwa, anakwenda kuandaa barua inayoonesha orodha ya mabonde ya kimkakati ya umwagiliaji yanayohitaji kuendelezwa na kuyatuma kwa kampuni ya Bergs & More, ili wayapitie na kuona fursa zaidi za uwekezaji nchini.
Pia, kikao hicho kilihudhuriwa na Mhandisi Anna Green Mwangamilo, Mkurugenzi wa Zana za Kilimo na Umwagiliaji Wizara ya Kilimo, pamoja na Bw. Daudi Kaali ambaye ni Mkurugenzi wa Mipango Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.