Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Mhe. Anthony Mavunde amesema kuwa serikali itawaunga mkono wawekezaji wote watakaokuja kufanya uwekezaji wa viwanda Jijini Dodoma kwani ujio wao utasaidia kuleta manufaa kwa wananchi kwa ujumla.
Pia, amewataka wakazi wa Dodoma kuwaunga mkono wawekezaji wanaokuja kuwekeza Jijini hapa kwani hiyo itasaidia kujenga na kuwainua kiuchumi na kuondokana na uduni wa maisha.
Mavunde ameyasema hayo mara baada ya uzinduzi uliyoambatana na uwekaji wa jiwe la msingi katika kituo cha mafuta cha Admire Oil Jijini Dodoma na kusisitiza juu ya wawekezaji kuendelea kuwekeza kwani bado fursa hiyo ipo.
Naibu Waziri huyo amesema kuwa eneo ambalo hivi sasa kituo hicho cha mafuta kimejengwa licha ya kuwa lilikuwa eneo la pori, itazalisha ajira nyingi kwa vijana hasa wakati huu ambapo serikali inaendelea na ujenzi wa miundombinu mbalimbali mkoani Dodoma.
Awali akizungumza katika hafla hiyo, msemaji wa makampuni ya Admire Oil Mohamed Ibrahim alisema kuwa, wamekuwa wakiajri vijana hasa wanawake ili kuondokana na kile kinachodaiwa ni kuwa na uduni wa maisha.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.