NAIBU Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jaffo ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa kutekeleza Sera na maelekezo ya Serikali kwa vitendo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa, asilimia 10 ya fedha zinazotokana na mapato ya ndani zinatengwa na kutumika kwa ajili ya kuwawezesha Wanawake na Vijana.
Naibu Waziri Jaffo ametoa pongezi hizo wakati akikabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 zilizotolewa na Manispaa hiyo kwa ajili vikundi vya Vijana na Wanawake katika hafla fupi ya makabidhianao iliyofanyika leo katika ukumbi wa Manispaa ya Dodoma.
Alisema Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma imeonesha mfano kwa vitendo na kwamba Halmashauri zingine zijifunze na kuiga, ambapo amedai hayo ni matokeo ya ushirikiano mzuri wa kazi uliopo kati ya Madiwani, Mkurugenzi, Wakuu wa Idara na Watumishi wote.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema fedha hizo zinatarajiwa kuvinufaisha vikundi 66, vikiwemo 18 vya vijana na 48 vya wanawake.
Alisema, Halmashauri hiyo imekuwa akitumia fedha za Mapato ya ndani kwa kuzingatia maelekezo ya Serikali ambapo pamoja na kutoa asilimia 10 kwa ajili ya vijana na wanawake, pia asilimia 30 inaelekezwa katika katika miradi ya Maendeleo ambapo mpaka sasa Kata 25 zimepatiwa sehemu ya fedha kwa ajili miradi ya maendeleo.
Aidha, Kunambi alisema kwa sasa Halmashauri hiyo inaanza kusajili vikundi vya walemavu ambavyo kwa mujibu wa Sera na Maelekezo ya Serikali vinatakiwa kupatiwa asilimia mbili ya Makusanyo ya fedha zinatokana na vyanzo vya ndani.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.