KITUO kikuu cha kuengesha malori kilichopo eneo la Nala (Nala lorry park) kimeanza kazi na kuwavutia wadau wa sekta ya usafirishaji ndani na nje ya Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru mapema leo tarehe 20 Januari, 2021 majira ya saa 11 alfajiri alifanya ziara ya kikazi kujionea hali halisi ya kituo kikuu cha kuegesha malori- Nala. Katika ziara hiyo, Mkurugenzi huyo aliridhishwa na utendaji kazi wa kituo hicho.
Kwa upande wake Mkuu wa Kitengo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Uhusiano katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Fungo alisema kuwa kituo hicho cha kuegesha malori ni mkakati wa serikali katika kutoa huduma bora kwa wadau wa sekta ya usafirishaji na wananchi kwa ujumla. Alisema kuwa baada ya kukamilika kwa kituo hicho, malori yote hayaruhusiwi kuegeshwa na kuzagaa katika jiji la Dodoma.
“Kituo cha kuegesha malori Nala kimekamilika, ni uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali ya awamu ya tano, hivyo, malori yote yanatakiwa kupati katika kituo kile. Madereva watakao kaidi utekelezaji huo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa taratibu zilizopo” alisema Fungo.
Akiongelea huduma za kijamii, mkuu huyo wa kitengo cha TEHAMA alisema kuwa tayari huduma mbalimbali zinapatikana katika eneo la kuzunguka kituo hicho. Miongoni mwa huduma zilizopo ni pamoja na usafiri wa aina mbalimbali, huduma za kijamii na chakula, aliongeza.
Kwa upande wake, mdau wa sekta ya usafirishaji ambaye ni dereva wa lori, Erenest Sangu alisema kuwa kutuo cha kuegesha malori- Nala ni kituo bora nchini. Kituo hicho kinawapa uhakika na usalama wa malori na mizigo yao kwa sababu eneo hilo limeimarishwa kiusalama, iliongeza.
Kituo kikuu cha kuegesha malori kimejengwa katika Kata ya Nala, jijini hapa kikiwa barabarani katika barabara kuu iendayo Singida umbali wa takribani kilometa 10 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma.
Mwonekano kutoka angani wa Kituo cha kuegeshea malori Nala.
Huduma ya usafiri wa chap chap 'bodaboda' inapatikana Nala Lorry Park.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.