• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Nala wanamchagua diwani wao tena leo

Imewekwa tarehe: September 19th, 2023

Na. Theresia Nkwanga, NALA

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Dodoma mjini, John Kayombo amewataka wakazi wa Kata ya Nala kujitokeza na kutumia haki yao ya kidemokrasia kupiga kura kumchagua mwakilishi wao.

Kayombo alisema hayo katika kituo cha Segu chini apokuwa akitoa muhtasari wa hali ya uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nala unaoendelea katika vituo 12 vya kata hiyo.

“Leo tarehe 19 Septemba, 2023 Kata ya Nala inafanya uchaguzi mdogo wa kuziba nafasi ya aliyekuwa Diwani ambaye alifariki. Zoezi la kufungua vituo lilifanyika kama sheria inavyotaka saa 1:00 asubuhi. Mpaka sasa saa 6 mchana zoezi la upigaji wa kura linaendelea vizuri na wananchi wamejitokeza kwa wingi kuja kuchagua mwakilishi wao. Niwaombe wananchi waendelee kujitokeza muda bado sasa ni saa 6 mchana hadi saa 10 jioni ndio tunafunga vituo” alisema Kayombo.

Aidha, aliwataka wananchi wakimaliza kupiga kura kurudi nyumbani. "Vituo vya kupiga kura baadae vinabadilika kuwa vituo vya kuhesabia kura. Mwisho matokeo ya kila kituo yatabandikwa kwenye mbao za matangazo kwa kila kituo. Baada ya zoezi hilo, wasimamizi wote wataondoka kuja kwenye kituo cha majumuisho ya vituo vyote kwenye Ofisi ya Afisa Mtendaji Kata ya Nala. Mshindi wa kiti cha Diwani Kata ya Nala atatangazwa leo na cheti cha ushindi kitatolewa leo” alisisitiza Kayombo.

Kuhusu hali ya upigaji kura, alisema kuwa wananchi wanapiga kura katika hali ya amani na utulivu. Tume ya Taifa ya Uchaguzi imejipanga vizuri kabisa.

Kwa upande wake Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Mhe. Mwanaisha Kwariko alisema kuwa hali ya vituo vya kupigia kuwa ni nzuri na vifaa vyote vilifika mapema na watendaji wote walikuwepo na ilipofika saa 1:00 asubuhi watendaji walikuwa tayari kuwapokea wapiga kura.

“Katika vituo vingi tulivyotembelea wapiga kura wengi walikuwa wameshafika kwa ajili ya zoezi hilo na wananchi walikuwa wakifuata maelekezo ya kujipanga kwenye mistari kwa ajili ya kupiga kura kwa utaratibu. Muitikio wa watu ni mzuri na watu wakishapiga kura wanaondoka. Hata wenye mahitaji maalum wanapokelewa na kuhudumiwa kama tulivyoelekeza wanapiga kura mapema na kuondoka” alisema Mhe. Kwariko.

Nae Mratibu wa Uchaguzi, Albert Kasoga alisema kuwa walijiaandaa vizuri kwa vituo vyote 12. “Kwa upande wa wasimamizi maandalizi yalifanyika na wote walipata mafunzo na wapo vizuri na wapo vituoni kama maelekezo yalivyokuwa” alisema Kasoga.

Mkazi wa Mtaa wa Chiwondo, Samwel Kusalo alisema kuwa zoezi hilo limeratibiwa vizuri. “Tulitangaziwa leo ni siku muhimu ya kutumia haki yetu ya msingi kupiga kura kumchagua diwani wetu. Nimekuja, nimepokelewa vizuri na wamekagua wakaona jina langu na nikatumia haki yangu ya msingi kupiga kura” alisema Kusalo.

Kata ya Nala yenye jumla ya wapiga kura 3,741 na vituo 12 vya kupigia kura inafanya uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekuwa Diwani wa kata hiyo Julius Chimombo aliyefariki tarehe 10 Aprili, 2023. Vyama vya siasa vinavyoshiki uchaguzi huo vikiwa 11.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.