MAONESHO ya Wakulima ya Nanenane 2020 Kanda ya Kati, yameacha alama nzuri na kubadilisha maisha ya wakazi wa Dodoma na maeneo ya jirani kwa kuwapatia elimu mbalimbali kuhusu Kilimo, Uvuvi na Ufugaji huku wakiipongeza Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kuwa mshindi wa kwanza.
Hayo yameelezwa na Wananchi waliokuwa wakitembelea maonesho hayo wakati wakitoa maoni yao baada ya kumalizika kwa Maonesho ya Nanenane ambayo Kitaifa yalifanyika Mkoani Simiyu na kwa Kanda ya Kati yalifanyika Mkoani hapa.
Kwa upande wake Richard Mtuyu Mkazi wa Nzuguni Dodoma amesema kuwa wanamshukuru Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma na timu yake kwani kupitia banda lao la Kilimo limewafanya wamejifunza mambo mengi yanayohusu kilimo cha kisasa kwani kabla ya hapo walikuwa wakilima bila utaratibu jambo ambalo lilikua likiwapatia hasara kwa mazao yao kushambuliwa na magonjwa na hata kupata mazao kidogo.
“Tunaishukuru sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma, maonesho haya yamefanyika faida kubwa sana kwetu hasa Wakulima wa Vijijini kwani tulikua tunapata tabu sana, unakuta mtu unalima zao fulani lakini mwisho wa siku unapata hasara kutokana na kutokua na elimu sahihi ya kilimo hicho” alisema Mtuyu.
Nae Elizabeth Mlacha Mkazi wa Kikombo, amezungumzia alivyojifunza namna ya kuandaa bustani za mbogamboga na kusema kuwa amejifunza kanuni za kilimo cha bustani, kitu ambacho kimembadilisha na baada ya elimu hiyo atakua ana andaa Bustani zake kisasa tofauti na ilivyokua awali.
“Mimi napenda sana kilimo cha bustani na nyumbani kwangu nina bustani za mboga, lakini tatizo lilikua ni namna ya kuitunza kitu ambacho kilikua kinapelekea bustani yangu kutostawi ila hapa nimekuta bustani zinapendeza na wamenielekeza namna sahihi ya kuandaa, kupanda na kuitunza bustani yangu kwa kweli nimefaidika sana tunashukuru” alizungumza Elizabeth Mlacha.
Maonesho ya Wakulima ya Nanenane 2020, yalianza tarehe 1/8/2020 na yalitarajiwa kumalizika tarehe 8/8/2020 lakini baadae Serikali kupitia kwa Waziri wa Kilimo Japhet Hasunga iliongeza siku mbili za maonesho hadi tarehe 10/8/2020, ili wananchi kote nchini wapate fursa ya kutembelea maonesho hayo.
Richard Mtuyu Mkazi wa Nzuguni Dodoma akiongea na mwandishi wetu kuhusu faida iliyopatikana kupitia maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati mwaka huu 2020 yaliyofanyika Nzuguni jijini Dodoma.
Kitalu cha kilicho bora cha Mahindi kwenye maonesho ya Nanenane.
Elizabeth Mlacha mkazi wa Kikombo akielezea alivyojifunza namna ya kuandaa bustani za mbogamboga na kanuni za kilimo cha bustani wakati wa Maonesho ya Nanenane Jijini Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.