• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

David Silinde azindua Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania (UWETA)

Imewekwa tarehe: November 6th, 2021

NAIBU WAZIRI Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), David Silinde amezindua Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania (UWETA) na kuwaagiza viongozi hao wakasimamie fedha za miradi ya maendeleo zinazopelekwa katika maeneo yao.

Naibu Waziri Silinde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na viongozi na wajumbe wa umoja huo ambao moja kwa moja ndio walengwa katika maeneo wanayoishi na wananchi kwa kuona na kusimamia maendeleo ya miradi inayopelekwa ujenzi wa miundombinu, huduma za kiuchumi na kijamii ikiwemo Elimu, Afya na Barabara.

Serikali inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan inatambua mchango na jitihada za Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji nchini zikiwemo pamoja na changamoto amesema Naibu Waziri Silinde, katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/22 Serikali imezitaka Halmashauri zote nchini kutoa fedha za ujenzi, kukarabati pamoja na ununuzi wa samani za ofisi hizo ili viongozi hao wawezE kutoa huduma bora kwa wananchi.

Akifafanua stahiki za viongozi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji amesema kuwa Serikali imeweka utaratibu kwa kila Mtaa au Kijiji kulipa posho kutokana na mapato yao. “Halmashauri zote nchini hupaswa kurejesha mapato ya Kijiji/Mtaa yanayojumuisha mapato yanayotokana na asilimia 20 ya mapato yanayokusanywa kutoka vyanzo vya ndani vya Halmashauri, nakiri kwamba utekelezaji wake unatofautiana kati ya Halmashauri moja na nyingine”. Amesema Silinde.

Aidha, amewaagiza viongozi wa umoja huo kuisaidia Serikali katika kushirikiana na Watendaji wa Mitaa, Vijiji na Vitongoji kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu ili kuzipa heshima Mamlaka za Serikali za Mitaa lakini pia kutatua changamoto za wananchi hasa migogoro ya ardhi nchini kwani hili linaanzia kwao.

“Hakikisheni mnaepuka kuwa chanzo cha migogoro ya ardhi katika maeneo yenu kwa kushiriki kuuza au kushuhudia uuzaji wa ardhi kwa mnunuzi zaidi ya mmoja na bila kuzingatia Sheria ikiwemo maeneo ya wazi, maeneo yaliyohifadhiwa au maeneo ya kingo za mito na bahari kinyume na Sheria” amesema Silinde.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania (UWETA), Lucas Mwasongwe ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao na kuiomba iendelee kuona umoja huo kwani wao wana nafasi kubwa kwa jamii katika kuleta maendeleo ya nchi.

Umoja wa Wenyeviti wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji Tanzania utaunganisha Wenyeviti wa Mitaa 4,263, Vijiji 12,318 na Vitongoji 64,361 nchini.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.